HATUA YA 324: Hakuna Anaejali, Kuliko Unavyotakiwa Kujali.

jacobmushi
By jacobmushi
3 Min Read

Ulishawahi kufanya jambo halafu matarajio yako yalikuwa ni watu wakuzungumzie au wakujali sana lakini ukaja kukuta hakuna hata anaehangaika na wewe? Hii inatokana na pale unapofanya jambo ili uonekane au usifiwe na mwisho wa siku unakuja kugundua kwamba wale ambao unawafanyia wala hawakufikirii.

Usije ukapoteza muda wako kufanya vitu ili upate sifa Fulani, au uonekane wewe ni mtu Fulani. Tafuta sababu za msingi na za muhimu za kukuvuta ufanye hicho unachotaka kufanya. Kama umeingia kwenye biashara ili upongezwe kama mfanyabishara bora kila siku utakuwa unaumia hasa utakapogundua kwamba hakuna mtu anaejali unachokifanya.

Fanya jambo uridhike wewe mwenyewe ndani yako na wala sio watu wa nje waridhike. Kuna msemo unasema hata uwe mwema kiasi gani kwa watu bado kuna watu watakuchukia tu bila sababu yeyote. Hii ina maana kwamba unapofanya kitu usifanye ili upate matokeo au sifa zozote kutoka kwa watu. Fanya kwasababu sahihi.

Ni sawa na mtu anaetoa msaada ili aje atajwe katika listi ya watu wanaotoa msaada sana. Mwisho wa siku utajikuta unaumia usipotajwa. Fanya kwasababu moyo wako umependa kufanya ili hata usipopongezwa na mtu yeyote uendelee kujisikia vizuri kabisa.

Fanya kwa bidii hata kama hakuna anaeona juhudi unazoweka. Endelea kupambana kama vile hakuna anaekutazama kwasababu kinachotakiwa kikutangaze ni matokeo ya juhudi zako na sio wewe mwenyewe.

Ukiishi Maisha ya kufanya vitu ili uonekane na watu utajikuta unaanza kufanya hadi vitu vya ajabu ili wat utu wakuzungumzie. Hupaswi kuwa mtu ambaye anafanya mambo kwa ajili ya kuwaridhisha wengine. Timiza yale majukumu yako hayo mengine waachie wanaohusika.

Kamwe;

Usifanye jambo lolote ili kuwaridhisha watu.

Fanya kwa ubora wa hali ya juu lakini sio kwa lengo la kuwaridhisha watu ila ni kwa ajili ya kutoa kitui bora.

Usifanye jambo lolote ili watu wakuone.

Fanya kwasababu umeamua kufanya ukionekana iwe ni matokeo yamesababisha ila halikuwa kusudi kuu la wewe kufanya.

Usifanye jambo kwa ajili ya kupata sifa

Fanya kwasababu ni majukumu yako, Fanya kwasababu unapenda kufanya.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading