Imekuwa ni kawaida sana kusikia watu wanasema biashara fulani inalipa sana au fursa Fulani ukifanya lazima utoke. Ndio inawezekana ni kweli ukifanya utatoka, mfano ni msimu ambao mahindi ya kuchoma yanahitajika sana mjini halafu hayapo. Ukiingia kwenye hiyo fursa na ukaweza kuyapata mahindi kwa bei rahisi ukaja kuyauza kwa bei ghali unajikuta umepata pesa ya maana.

Ubaya wake ni kwamba ili uweze kufanya biashara hizi na utoke lazima uweze kupiga mahesabu sawasawa la sivyo unaweza pia kupiga hasara. Mfano umeona nyanya imepanda bei sana sokoni halafu wewe ukakimbilia kwenda kulima kumbe mlikimbilia wengi kulima na hivyo wote kujikuta mnavuna kwa wakati mmoja na kusababisha bei ya nyanya kushuka na wote mkapata hasara.

Ukweli kuhusu biashara ambazo wengi wanakuwa wanasema zinalipa huwa hazidumu. Zinakuwa kama bahati nasibu Fulani hivi ambayo ukichelewa basi unapata hasara. Sasa kama na wewe Rafiki yangu umekaa unasubiri upate biashara inayolipa sana unakuwa huna tofauti na mtu anaesubiria bahati nasibu.

Ukishaanza kuona kitu watu wamekinadi sana ujue kuna kupata hasara kama utaingia kichwakichwa. Ni vyema ukajua kwamba biashara yeyote inalipa unachopaswa wewe ni kuhakikisha upo kwenye biashara na unafanya kwa bidii na ubunifu. Huko kulipa kukifika kukakukuta upo kwenye biashara  utatoka tu.

Mfano wewe ni umeamua kuwekeza kwenye kilimo cha mahindi bila kujali kama unapata faida kubwa sana wewe endelea tu kupata kile unachostahili. Ikitokea siku mahindi yamekuwa adimu sokoni moja kwa moja na wewe utaingia kwenye watu ambao watafaidi. Lakini ukikaa nje unangojea watu waanze kusema biashara Fulani inalipa sana kipindi hiki utaishia kujuta na kupoteza pesa zako.

Hakikisha kuna kitu unakifanya usiwe mtu ambaye umekaa tu unangojea biashara inayolipa sana ije ndio uingie. Wakati wako wa kutoka ukifika utatoka tu haswa kama ulikuwa unafanya kazi kwa bidii.

I will prepare and someday my chance will come.” – Abraham Lincoln

Huu ndio msemo ambao unatakiwa uufanyie kazi. Wewe jiandae na fanya kazi kwa bidii siku yako inakuja, utakutana na fursa itakayokutoa. Acha kukimbizana na fursa wewe endelea kujiandaa kwa kufanya kazi kwa bidii.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading