Kwenye dunia ya sasa ya mitandao ya kijamii imekuwa ni rahisi sana kuweza kumtafuta mtu yeyote na kuona mambo mbalimbali anayoyafanya. Ni rahisi sana kujua vitu kuhusu watu hao lakini sio rahisi kuujua ukweli kuhusu wao.

Watu wengi wamekuwa wanatengeneza picha mbalimbali za watu kutokana na yale walioona kwenye mitandao. Ni rahisi kutengeneza picha Fulani kuhusu mtu kwasababu ya picha ulizoona kaweka kwenye mtandao na ukaja kukutana nae ukakuta ana Maisha tofauti kabisa.

Unachotakiwa kujua ni kwamba yale yanayoonekana ni sehemu tu za Maisha ya watu. Bado kuna mengi hutayajua kuhusu watu kwa kupitia kwenye mitandao ya kijamii. Unaweza kufikiri mtu huyu ana furaha siku zote kutokana na picha anazoweka kumbe ni mtu mwenye huzuni sana kuliko hata wewe. Ukweli halisi juu ya Maisha ya mtu anaujua yeye.

Ni kweli hutakiwi kuyaweka Maisha yako wazi mbele ya kila mtu ndio maana pia wengi hufanya hivyo. Cha muhimu ni kutokudanganya watu aina ya Maisha ambayo unaishi kumbe sio uhalisia. Sio lazima uweke kila kitu kwenye mitandao onesha tu kile ambacho kila mtu anapaswa kuona na sio yale ambayo wewe na watu wako wa karibu tu mngepaswa kuyajua.

Jambo la muhimu unalopaswa kulitambua ni kwamba kila unachokiona kwenye mitandao kinachohusu Maisha ya watu ni kile ambacho wameamua wewe uone. Kuna mengi Sana ambayo hutayajua kuhusu wao kwasababu hawataki uone.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading