HATUA YA 327: Mbinu Ya Kuweza Kufanya Usiyoyapenda.

By | April 18, 2018

Tunasema ili ufanikiwe ni muhimu ukafanya kile unachokipenda. Ni kweli hili kabisa ila sasa katika kufanya kuna mambo utakutana nayo ambayo huyapendi kabisa. Hayo mambo yanaweza kuwa ya muhimu sana katika kufikia mafanikio.

Mfano unafanya unachokipenda na lakini kinakulazimisha uamke mapema saa kumi. Hapo wewe unapenda sana kulala, itakubidi uamke mapema japokuwa unapenda kulala.

Unapenda kufanya biashara lakini unaogopa au hupendi kuzungumza na watu. Inakubidi ili uweze kufikia mafanikio kwenye biashara ujifunze sana kuongea na watu hata kama hupendi.

“Everybody should do at least two things each day that he hates to do, just for practice.” -William James

William James, Mwandishi wa Kitabu bora sana kiitwacho As a Man Think, alisema “kila mmoja anapaswa kufanya angalau mambo mawili anayoyachukia kila siku, kama mazoezi” (sio tafsiri halisi). Yaani kuna mambo japokuwa unayachukia ni lazima uyafanye ili uweze kufikia mafanikio.

Hupendi kusoma vitabu lakini mafanikio yanataka watu ambao wanatafuta maarifa, jifunze kusoma vitabu. Hupendi kuamka mapema ndio lakini mafanikio yanakulazimisha uamke mapema. Jifunze kuamka mapema.

Hupendi kuweka akiba, na unataka uhuru wa kifedha, huwezi kuupata kama hutajilazimisha kuweka akiba.

Yapo mambo mengi sana tunapenda kufanya lakini katika kuyafanya inatupasa tupitie katika njia ambazo hatutaki kupita. Inatubidi tufanye mambo ambayo tulikuwa tunayachukia sana.

Ni jukumu lako kuandika yale mambo ambayo unajua kabisa huyapendi au ni kama kero kwako lakini yana mchango fulani kwenye mafanikio halafu uanze kufanyia mazoezi kila siku.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
https://jacobmushi.com/patavitabu/

One thought on “HATUA YA 327: Mbinu Ya Kuweza Kufanya Usiyoyapenda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *