Mtoto mdogo anapofanya jambo la tofauti na alilozoea kufanya na akafanikiwa mara nyingi hupenda kwenda kwa mzazi wake na kumwonyesha huku amejawa na furaha sana. Inaweza kuwa ni mtihani shuleni au majukumu aliyopewa kutekeleza. Lakini tukija kwenye uhalisia kufaulu mtihani shuleni kwa mtoto ndio jukumu lake hasa. Anakwenda shuleni kusoma na kujifunza ili afaulu.

Tunapokuja kwa watu wazima kuna ambao wamekuwa na tabia ya kufanya vitu kwenye Maisha yao na kuvifanya kama maonyesho. Ukweli ni kwamba unakuwa na tabia kama za mtoto yule aliefaulu masomo au aliemaliza kazi aliyoagizwa na mzazi. Tofauti ni kwamba wewe huna mtu maalumu wa kwenda kumwonyesha Zaidi utapost kwenye mitandao ya kijamii.

Unapofanya jambo lolote la maendeleo kwa ajili ya Maisha yak ohayo ni majukumu yako. Yaani ndio ulipaswa haswa ufanye hivyo, sio kwamba umefanya jambo la kishujaa sana.

Unapofanya wema kwa wengine, ni jukumu lako wewe kama mwanadamu kuwafanyia wema wanadamu wenzako. Acha kupoteza muda kuwaonyesha watu endelea kufanya mengine mengi Zaidi.

“As a horse when he has run, a dog when he has tracked the game, a bee when it has made the honey, so a man when he has done a good act, does not call out for others to come and see, but he goes on to another act, as a vine goes on to produce again the grapes in season.”
― Marcus AureliusThe Meditations of Marcus Aurelius

Mwanafalsafa huyu anatuambia kwamba farasi anapokimbia, mbwa anapokuwa kwenye michezo yake, au nyuki anapotengeneza asali yote hayo ndio majukumu yao. Walizaliwa waje kufanya hivyo, miti ya matunda imekuwepo ili itoe matunda. Haihitaji kusifiwa au kuonekana na watu ndipo iendelee kwa bidi kutoa matunda.

Sasa wewe kama mwanadamu umezaliwa ili uje kufanya matendo mema. Umezaliwa ili uliishi kusudi lako usisubiri mtu akusifie au akuone ndipo upate nguvu ya kufanya. Wewe endelea kutimiza kusudi, wapo wengi wanafurahia sana uwepo wako hapa duniani hata kama hawajasema. Usipoteze muda kabisa kusubiri kusifiwa au kuonekana na watu.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading