“We suffer more often in imagination than in reality”
― Seneca

Mara inaweza kuwa jambo dogo sana limetokea mahali lakini kwa kupitia fikra zetu tukajikuta tumekuza lile jambo na kuendelea kupata maumivu makubwa. Mwanafalsafa Seneca anasema tunateseka Zaidi katika vitu tunavyovifikiria kuliko vile vitu halisi. Mfano mdogo ni pale umempigia mtu simu hakupokea au akaikata unaweza kutengeneza majibu yako mwenyewe kwenye kichwa kwamba yule mtu ana dharau, hakuheshimu, haheshimu simu zake, hakupendi, hakujali, na mengine mengi.

Lakini sasa ukweli unaweza kuwa ni tofauti kabisa na hayo uliyokuwa unayawaza wewe. Inawezekana kabisa huyo uliyempigia simu alikuwa yupo kwenye kikao, au simu ilikuwa mbali na yeye, au yupo kwenye maongezi ya muhimu sana ambayo asingeweza kuacha na kupokea simu. Sasa kwasababu tu wewe hujaelewa ukweli huu unaweza kujikuta unateseka ndani ya  moyo wako. Wengine hata machozi hutoa, wengine na matusi pia hutoa.

Ili uweze kuwa salama katika fikra zako jaribu kuchukulia karibu kila jambo kwa mtazamo chanya. Hasa yale mambo ambayo huna ukweli nayo wa moja kwa moja. Ukishindwa unaweza kujikuta unateseka sana ndani ya moyo wako. Unaweza kufikiri Fulani hakupendi wala hakujali lakini yeye binafsi anakupenda sana na anakujali sana.

Tengeneza fikra chanya kwenye kila tukio. Usitoe hukumu kwa jambo lolote ambalo hujui upande wake wa pili ukweli ni upi. Usijiingizie maumivu na mawazo potofu bila kujua undani wa kile ambacho umekiona au kimetokea.

Fikra zetu tukishindwa kuzitumia vizuri sisi tunaweza kuwa watumwa wa fikra zetu.

Siku zote:

Usihukumu Usichokijua.

Usimchukie mtu kwasababu yeyote ile.

Usiweke kinyongo wala kisasi.

Jambo lolote linalokuumiza na Kuna mtu unaweza kumuuliza nenda kamuulize akusaidie usibaki unateseka ndani ya moyo wako. Ukiona kuna kitu kinakupa mawazo, tafuta mtu unaemuamini muulize. Hata kama unahisi kuna usaliti ndani ya mahusiano yako badala ya kuendelea kuumia mwenyewe ndani ya moyo wako tafuta mtu ambaye unamwamini muulize. Utajikuta unatoka kwenye vifungo vibaya ndani ya moyo wako.

Kwasababu ya fikra hizi tunazozijenga ndani ya mioyo yetu kuna wengi wamejinyonga, wengine wamekunywa sumu. Usikubali kufikia mahali kujidhuru kwasababu ya maumivu unayopitia ndani yako. Usikubali kukonda tafuta mtu wa kukusikiliza Maisha yako yana thamani kubwa sana usiyapoteze kwa kufikiria kitu ambacho kinakuumiza.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading