Katika Maisha yetu ya kila siku na vitu tunavyofanya kuna kitu ambacho tunatengeneza. Vile unavyoishi Maisha yako kuna picha watu wanaijenga kuwa wewe ndio hivyo ulivyo. Vile unavyoongea kuna picha watu wanajenga kwenye akili zao kwamba wewe ndio hivyo upo.

Kama unaongea maneno ya hovyo picha itakayojengeka ni kwamba wewe ni wa hovyo. Kama utakuwa unazungumza kwa busara watu watajenga picha kwamba wewe ni mtu wa busara. Kama unakuwa wa kujibu jeuri watajenga picha kwamba wewe ni mtu jeuri. Kama unaishi Maisha yasiyoeleweka bado watu watakupa tafsiri.

Leo nataka Rafiki yangu ukae utafakari Maisha yako ya kila siku. Je unatengeneza picha gani kwenye Maisha ya watu. Hawa watu ndio wanaweza kuja kuwa wateja wa bidhaa yako, wanaweza kuja kuwa watu ambao watafungua njia mbalimbali kwenye Maisha yako. Yale unayoyaonyesha mbele yao leo yatakufanya wajenge picha ya namna gani vichwani mwao?

Jiulize tena kwa Maisha unayoishi unajijengea ukuta au unafungua njia? Tabia zako zinaweza kuwa zinakujengea ukuta ndio maana fursa huzioni. Ndio maana umekuwa unakwama mahali na hakuna mtu wa kukusaidia. Watu wameshakuona wewe ni msumbufu kwenye mambo ya fedha hawataweza kukupatia pesa zao tena. Wakishaona unaongea sana huna vitendo watabaki na picha hiyo hiyo.

Nina amini kweli kabisa huwezi kuishi Maisha ya kumridhisha kila mtu ila unaweza kuishi Maisha bora. Maisha ambayo yatakuwa na faida kwako wewe na kwa wengine. Mdomo wako utoe maneno ya baraka kwa wengine. Matendo yako yawe na mchango chanya kwenye Maisha yako na Maisha ya wengine.

Kama hutoamini wewe jaribu kujiuliza ni vitu gani watu wanasema juu yako wakati wewe haupo? Kile wanachokisema kuhusu wewe ni hicho walichokiona kwenye Maisha yako. Wanachokisema ndio picha waliojinga kuhusu.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading