HATUA YA 334: Ukitaka Kuwa Mkubwa wa Wengine Kubali Hiki..

jacobmushi
3 Min Read

Kanuni ya kuwa Mkubwa wa wengine siku zote ni kutumika. Hakuna bosi alieweza kuajiri maelfu ya watu kwenye kampuni yake kama hakutoa muda wake akitumika hadi akafikia uwezo wa kuajiri. Hakuna aliefikia mafanikio makubwa na kujulikana na wengi kama hakutoa nguvu zake katika kuonyesha ule uwezo uliokuwa ndani yake.

Hata kama una sauti nzuri ya kuimba kuliko wote hapa duniani kama hutajitoa na kuanza kuimba hiyo sauti peke yake haiwezi kukufanya uwe muimbaji mashuhuri. Lazima ukubali kutumika, utoe nguvu zako, uweke juhudi, na wakati mwingine udharauliwe. La sivyo utabakia na sauti yako nzuri.

Ukitaka kuwa mkuu lazima ukubali kunyenyekea, ukubali kufanya kazi kwa ajili ya wengine. Lazima wakati mwingine ukubali kuonekana mjinga. Watu wengi wenye mafanikio ya kudumu mwanzo wao walikuwa wanafanya kazi kubwa kwa ajili ya watu. Hata sasa bado wanafanya kwa ajili ya watu.

 

Mathayo 20:26b; Yesu akawaambia “bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu;”

Ukitaka kuwa wa kwanza lazima ukubali kutumika kwa ajili ya wengine. Chochote kile unachokifanya lazima kiwe kinagusa Maisha ya wengine. Kuna wakati ili ufanikiwe unapaswa kusahau shida zako na kuziangalia Zaidi shida za wengine. Kuna nyakati ili uweze kufanikiwa wewe unapaswa kujinyima kwa kiasi ili wengine wapate.

Kuna sehemu huwezi kufika kama hujawafikia watu na kubadilisha Maisha yao. Kuna sehemu kazi zako zinapaswa zianze kukutangulia wewe ndipo wewe uje nyuma. Tatizo la wengi tunapenda kuonekana sisi kabla kazi zetu hazijaanza kuonekana. Unajua kabla watu hawajamjua mwimbaji ni nani wanaanza kusikia nyimbo yake.

Ili watu waanze kutafuta habari ni mpaka wasikie kazi zako. Hadi waone matokeo ya kazi zako. Mimi nilianza kufuatilia juu ya Tajiri Mo Dewji baada ya kutumia bidhaa zake. Kama unataka kuwafikia watu anza kutanguliza zile kazi zako kwanza kisha wewe uje nyuma. Watu watakuita tu baada ya kuona kazi zako.

Weka mbele Zaidi maslahi ya wengine na hapo utakuwa umeyagusa maslahi yako moja kwa moja.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading