Kwenye dunia hii ambayo kila unachotaka kuwa unaweza kuwa ni vyema ukachagua kuwa mwema. Hii ndio njia pekee ya kwanza kuonyesha wewe ni binadamu. Mtu anapofanya jambo baya la kikatili kuna usemi hutumika “amefanya jambo la kinyama sana” yaani maana yake wewe kama binadamu tofauti yako na Wanyama wengine ni ule utu ulioko ndani yako.

Mtu mmoja akasema kama duniani umetafuta na hujaona mtu mwema hata mmoja basi kuwa wewe. Yaani anza kufanya wema, ishi Maisha mema, usitafute mtu au watu wema badala yake anza wewe kuwa mwema. Wema wenzako watakufuata.

Kinachotuharibu wanadamu na kutufanya tufanane na Wanyama ni ubinafsi. Unajua kitu pekee anachofikiria mnyama wa porini ni kula na kuzaliana tu. Yeye hawazi pa kulala, hawazi kusomesha, hawazi kugundua chochote, hawazi kusafiri. Kwasababu ya kukosa haya anakuwa mar azote anachokifikria ni kuhusu yeye peke yake.

Wewe mwanadamu una mengi ya kufanya. Bahati nzuri sana ni kwamba ili uweze kujisaidia wewe lazima uwe umewasaidia wengine. Ili upate chakula lazima uende kwa mtu anaehitaji nguvu kazi yako, ujuzi wako au kile ambacho unacho mbadilishane. Sio kama Wanyama ambao wakati mwingine hunyang’anyana uhai ili waweze kuendelea kuishi.

Wewe mwanadamu ili uweze kuishi kwa Amani na furaha kuwa mwema kwa kuanza kutumia kile ulichopewa na Mungu kwa ajili ya wengine. Hakuna namna nyingine unayoweza kuwa mwema Zaidi yah apo. Kitendo cha mtu aliepewa uwezo wa kugundua simu ni wema wa hali ya juu. Angeweza kukaa kimya na kusema sio lazima nifanye. Wewe una nini ndani yako? Toka anza kuchukua Hatua sasa inawezekana.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading