Unapoona mabaya yamekuja kwako usiwe mwepesi wa kulalamika bali penda kujiuliza maswali. Penda kudadisi ni wapi umekosea au ni kitu gani unapaswa kujifunza.

Umeingia kwenye mahusiano na mtu na mkajikuta mnashirikiana kwenye mambo mengi kwa pamoja. Maono yenu mkaweka pamoja, na baadhi ya mambo mkaanza kufanya pamoja. Mnakuza vitu pamoja hadi mnafikia Hatua ya kubwa kubwa. Ghafla yanatokea ya kutokea mnajikuta mmeachana na kila mlilokuwa mnafanya pamoja linashindwa kuendelea tena.

Mambo kama haya yamewakuta wengi sana na wanajikuta wanaharibika badala ya kujengeka na kuwa imara Zaidi. Unapaswa kuwa unajiuliza maswali mara kwa mara kwanini hili limetokea? Mungu anataka kunifundisha nini? Natakiwa niende wapi? Ni kweli unaweza kuvunjika moyo na kukosa Imani kabisa na watu lakini hilo sio suluhisho.

Unapaswa kubeba majukumu yako linapotokea swala la kuvurugika kwa mahusiano.

Kubali kwamba Ulikosea.

Yametokea yaliyotokea usiojione wewe huna makossa hata kidogo yeye ndiye aliekusaliti. Unajua hata kumchagua tu basi ulikosea. Hivyo usiseme kwamba huna makossa yeyote. Orodhesha madhaifu yako yote na uyafanyie kazi achana na madhaifu yake kwasababu ameshaondoka kwako.

Usitupe Lawama kwa Mtu

Adamu alipoulizwa na Mungu ni kwanini umefanya haya? Akatupa lawama kwa Hawa eti kwamba ndiye aliempa tunda ale. Ukweli ni kwamba Adamu alitakiwa akubali kwamba alifanya makossa kwa kutokutii maagizo. Yeye ndie alikuwa na uwezo wa kusema hapana tusile tunda hilo.

Usiseme Sitapenda tena bali Jiulize Kuna Kitu gani unatakiwa ujifunze.

Usichukie mtu yeyote.

Kuna hali ya kusema nawachukia wanawake wote, ooh nawachukia wanaume wote. Ooh wanaume wote ni sawa tu. Hilo ni jambo bay asana kwasababu unajitabiria ubaya uendelee kutokea kwako endapo utakuwa na mtu mwingine. Duniani kuna watu Zaidi ya bilioni 7 sasa wewe usiseme watu wote wako sawa kwasababu ya hayo uliyoona kwa watu wawili au watatu tu.

Songambele.

Mtu yeyote aliendoka kwenye Maisha yako haijalishi alikuwa mzuri kiasi gani, haijalishi ulimpenda kiasi gani, Kitendo cha kuondoka ni kwamba hakupaswa kufika kwenye hatma yako pamoja na wewe. Unapaswa ujue kwamba wa kwako yupo ndio maana huyo ameondoka. Kuendelea kubaki na maumivu ni kujecheleweshea kumpata yule ambae alipaswa kuwa wako.

Kuwa Mpya Kila Siku.

Mtu mmoja akasema ukitaka mtu bora kuliko yule ambaye ulikuwa nae basi jitengeneze wewe uwe bora Zaidi ya wakati uliokuwa nae. Moja kwa moja atakuja mtu ambaye ni bora kuliko yeye. Unachopaswa kufanya ni kuhakikisha unakuwa mpya kila wakati. Usikubali kuwa yule yule alieachwa mwaka jana.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading