Kwenye Maisha unapaswa uweze kutofautisha kati ya vitu ambavyo unatakiwa uvifanye vitokee na ambavyo unatakiwa usubiri vitokee kwa uweza utokao juu.

Ukishindwa kuvitofautisha hivi unaweza kukuta unateseka sana kwenye mambo ambayo ulipaswa kufanya mwenyewe. Unapoteza muda kwenye vitu ambavyo havipo kwenye uwezo wako wa kuvifanya vitokee.

Ukiwa na vipaji vizuri vya uchoraji ukachora picha ukaziweka ndani hakuna atakaeziona hata kama ungechora vizuri kiasi gani. Lazima ujue kwa kuonyesha ndio kunafungua nafasi ya wewe kupata fursa Zaidi.

Usikubali kukaa sehemu unasubiria nafasi zitokee kuna nyakati zinatakiwa zifike uwe na uwezo wa kutengeneza nafasi hizo. Wewe umependa binti badala ya kumwambia ukasema unasubiri itokee nafasi ya nzuri ya kuongea nae, na wakati huo huo kuna wenzako wanatengeneza nafasi za kuongea nae. Maana yake wewe unaesubiri nafasi zitokee zenyewe utajikuta umechelewa.

Usiendelee kusubiri nafasi itokee Rafiki yangu jitokeze wewe, onyesha kile kilichopo ndani yako watu waone na nafasi zitatokea. Ukikaa ndani umejifungia wewe na uwezo wako utajikuta unaendelea kulalamika hakuna nafasi hakuna fursa.

Usiogope kuchukua Hatua usingojee nafasi zitokee pale unapotakiwa ugonge mlango. Fanya kazi kwa bidii, na nafasi za wewe kufanikiwa zitakukuta kazini.

 

 

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading