Kitu cha kwanza kinachowapoteza wengine na kuwafanya wengine wafanikiwe ni marafiki.
Marafiki wana nafasi kubwa sana katika kuamua hatma yako, hii ni kwasababu maamuzi mengi unayoyafanya yanategemeana na marafiki zako wanafanya nini na watasemaje.
Kama una marafiki ambao mara zote wanawaza kushindwa na hakuna chochote wanachojaribu hawa ni wa kukaa nao mbali.
Kama marafiki zako hawana maono watakupoteza tu hakuna namna nyingine. Yaani maana yake hawana sehemu wanayoelekea hivyo lazima mpotezane. Kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake.
Kama marafiki zako mar azote mkikaa pamoja wanaleta hadithi zisizo na maana. Hawana mawazo chanya yanayoongeza ufahamu wako ni lazima utapotea tu. Kwasababu hawa ndio watu unaowaamini, ni watu walioshikilia sehemu ya Maisha yako.
Katika mambo magumu ambayo watu wengi wanapitia ni namna ya kuchagua marafiki. Hii inatokana na watu wengi hawajitambui kama hujitambui huwezi kujua ni nani wa kuambatana nae.
Kitu Cha Kufanya:
Hakikisha umetambua wewe ni nani, hakikisha umekua na maono. Tengeneza picha kubwa ya kule unapokwenda na unakotaka kufika. Hakikisha umejua ni wakina nani wa kuambatana nao. Hakikisha unajua ni wakina nani wakukaa nao mbali.
Ni ngumu sana kuachana na rafiki mlietoka nae mbali lakini chagua mwenyewe kupotea au kuwa na Maisha yako. Ukimaliza safari yako hapa duniani utahesabiwa wewe kazi uliyofanya sio marafiki. Fanya maamuzi sahihi kwa ajili ya Maisha yako.
Soma: Hichi Ndicho cha Kujivunia

Kuna mambo mengi yanaweza kuwa hayaendelei kwenye Maisha yako kwasababu tu ya aina ya marafiki ulionao.

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading