Huwezi kusema unataka mwili wenye misuli bila ya mazoezi magumu na mazito. Huwezi kusema unataka mtoto lakini hutaki kubeba majukumu ya kupata mtoto. Maumivu, kukataliwa, kupingwa, kusemwa vibaya, kuonekana umechanganyikiwa ni dalili zinaonyesha kwamba kile unachokifanya kina matokeo makubwa sana na hakijawahi kufanywa na wengine.

Dalili ya kwanza ya kujua kule unapoelekea ni kwa namna gani ni aina ya changamoto unazopitia. Kila changamoto ina maana yake katika safari yako ya mafanikio, kuna sehemu huwezi kufika kama hujapitia kwenye changamoto. Kuna sehemu hutaweza kusimama kama hujapitia kwenye changamoto Fulani.

Kama ambavyo ilivyo jeshini vyeo havipatikani kwa kuhongwa au kupendelewa bali kwa kufuzu mafunzo ndivyo pia katika mafanikio. Ukipokea kwa njia haramu lazima utakuja kuharibu tu. Hata matendo yako yataonyesha kwamba sehemu uliyopo imekuzidi ufahamu na uwezo.

Kuna Maisha huwezi kuyafikia na ukayaishi kwa uhuru kama hujapitia kwenye changamoto Fulani. Mfano wewe umeanza biashara na hujawahi kupata hasara yeyote ile na biashara inakua tu kila siku. Ni kweli unaweza kuona unafanya vizuri ila kwa upande mwingine hiyo inaweza kuwa dalili mbaya. Kuna sehemu utafika utakuwa unaishi kwa hofu kubwa ya kupoteza kwasababu hujawahi kupoteza hata kidogo.

Katika kupoteza tunajifunza kuna kupoteza na tunakuwa na nidhamu katika vile tulivyovipata. Kama uliachwa unajifunza kuna kuachwa hivyo uwe na umakini katika yule ambaye umekuwa nae au unaemtaka. Umetapeliwa basi unajifunza kwamba unatakiwa kuwa makini na watu na pia katika kila unalolifanya.

Hivyo ndivyo yalivyo mafanikio, hayajapishana sana na changamoto, ni kama vile zilivyo sifuri katika bilioni moja. Wakati ukiwa shuleni ukipata sifuri kwenye mtihani unaonekana umefeli na mjinga kuliko wote. Lakini huku mtaani kwenye Maisha unahitaji sifuri nyingi Zaidi ili uweze kuitunza vizuri bilioni yako.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

One Response

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading