Kila mmoja anatamani sana kwenda na wakati, hakuna anaetaka kuonekana yeye ni wa zamani. Hii ndio maana unakuta watu wanakimbizana na mitindo mbalimbali mipya ya mavavi. Simu mpya, magari mapya na vitu kadha wa kadha. Tatizo linakuja pale ambapo unajitahidi sana uende na wakati kwa nje lakini unasahau ndani yako.

Unaposahau ndani ukabaki unapamba nje ni sawa na nyumba ambayo ndani ni chafu sana lakini nje imepakwa rangi mpya na nzuri sana. Ndani kuna kila aina ya takataka lakini nje kumezingirwa na bustani nzuri zinazovutia.

Watu wanatamani sana kuwa karibu na wewe ili wajifunze vitu kutoka kwako kwasababu wameona unakwenda na wakati na kila kitu kizuri unacho. Cha ajabu wakifika kwako wanakuta wewe ni mtu wa ajabu sana. Umejaa dharau, majivuno mengi, huna hata neon zuri la kumtia moyo mtu. Hii ni kwasababu nje unavutia lakini ndani ni pachafu.

Wengi wengi tungezijali akili zetu kama ambavyo tunajali miili yetu na muonekano wetu wa nje basi tungekuwa tumefika mbali Zaidi ya hapa tulipo.

Ushauri wangu kwako ni uwekeze nguvu nyingi na pesa nyingi katika kukuza ufahamu wako Zaidi ya kitu kingine chochote. Hii ni kwasababu katika vitu ambavyo unataka kumiliki kwa nje ili uonekane unakwenda na wakati hakuna hata kimoja kinachotengenezewa nchini kwako. Na hata kama kipo basi ni kimoja au viwili. Jitahidi sana kwenda kwako na wakati kuwe ni kuanzisha biashara mpya, kuwasaidia watu kadhaa waweze kuvuka changamoto, kuanzisha jambo kwa ajili ya wengine.

Kwenda na wakati kuwepo katika akili yako, uweze kusoma vitabu, mara kwa mara. Penda kujifunza, uende na wakati katika akili yako pia. Usipendeze tu nje pendeza na ndani ya akili yako na pia kwenye moyo wako.

Ukiweza kwenda na wakati katika sehemu kuu za Maisha yako basi wewe unakuwa unaishi Maisha yenye furaha na mafanikio. Hakikisha roho yako inakwenda na wakati, hakikisha akili yako inakwenda na wakati. Hakikisha pia mwili wako, afya yako inakwenda na wakati.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading