Dada mmoja alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni kubwa sana sehemu ya mapokezi. Kazi ile ilimpa kiburi sana kwasababu ilikuwa ni kampuni ambayo ina jina kubwa sana. Alikosa adabu kabisa kwa watu ambao hawajui ana alionyesha dharau waziwazi. Kwa unafiki mkubwa alijifanya anawahudumia vizuri sana wale watu wakubwa ambao aliwajua majina na vyeo vyao.

Baada ya miaka kupita  akapata matatizo kwenye kazi yake na akafukuzwa. Hali ile ilimuumiza sana kwasababu alikuwa anaitegemea kazi yake kwa asilimia mia moja. Hakuwahi kuwaza kuipoteza kazi yake kwasababu tayari alishakuwa na mahusiano mazuri na bosi wake.

Akaanza kutafuta kazi nyingine taratibu. Kitu cha kushangaza ni kwamba karibia sehemu zote alizokuwa akipeleka barua za maombi alikutana na mojawapo ya watu aliokuwa anawaonyesha dharau ndio mabosi tena ambao wanahusika kwa kiasi kikubwa katika kutoa ajira. Aibu zilikuwa zinamshika na akashindwa kufanya chochote mbele ya watu wale. Mwishoni kabisa alikata tamaa kwasababu jina lake lilikuwa ni baya mbele za watu wengi.

Hii inatufundisha kwamba matendo yetu ya leo ni matokeo  ya kesho yetu kubwa. Huhitaji kujua vitu vingi sana ili uweze kufanikiwa kwenye baadhi ya mambo unatakiwa ujue kuishi na watu vizuri. Watendee wengine mema hadi siku una jambo lako wenyewe waone aibu kukuacha hivi hivi wajitoe wenyewe kwa ajili yako.

Kuna mengi tunafanya mazuri na mabaya bila kujua kwamba matokeo yake ni makubwa kwenye Maisha yetu ya baadae. Kuna wateja wako utakuja kuwahudumia baadae kama utaweza kutengeneza jina zuri kwenye kazi yako ya sasa. Kuna maadui pia utakuwa unatengeneza endapo utashindwa kuishi vizuri na watu.

Vitu vizuri ulivyopewa ni kwa ajili ya wengine hakikisha unakuwa baraka kwa wengine na sio kikwazo. Kufanikiwa kwako wewe ni ili uwe daraja kwa wengine wanaotaka kupita hapo ulipowekwa wewe.

Ipo siku usio ijua matokeo ya matendo yako yatajitokeza mbele yako, inaweza kuwa ni aibu kubwa au furaha sana. Yote inategemea na unachokifanya sasa.

 

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading