Kama kuogopa kwako hakubadilishi chochote kwenye kile unachokiogopa hakuna maana ya kuogopa. Hakuna haja yeyote ya kuwa na woga ama wasiwasi kwasababu hakubadilishi matokeo yeyote katika yale tunayoyaogopa.

Kama umeambiwa mafanikio sio rahisi na ukaingia huku una hofu kubwa na mawazo juu ya ugumu ni sawa na kupoteza nguvu zako bure kwasababu kuogopa huko hakubadilishi chochote. Unachopaswa kufanya ni kuangalia yale yaliyo ya muhimu katika safari yako.

“If you believe that feeling bad or worrying long enough will change a past or future event, then you are residing on another planet with a different reality system.” -William James

Ukiingia kwenye mahusiano ukiwa na hofu ya kuachwa au kuumizwa unakuwa unapoteza nguvu zako bure tu. Ni bora ungetumia nguvu hizo na muda huo wa kuhofu katika kujifunza. Hakuna maana ya kupoteza muda katika vitu ambavyo havibadilishi matokeo yeyote katika Maisha yetu.

Ni kweli hofu ipo huwezi kuiondoa bali unaweza kupunguza muda unaotumia kuhofia vitu ukaenda kufanya vitu vingine. Ukimuona simba yuko mbele yako na unajua kabisa anakula watu wewe kubaki umehofu na kutetemeka bila kufanya chochote haibadilishi yule simba, hawezi kukuonea huruma kwasababu unatetemeka. Labda ujaribu kumtishia kidogo.

Changamoto tunazishinda kwa kuwa imara na wajasiri na sio kuwa na hofu. Hofu ndio inaongeza nafasi ya kushindwa jambo kwasababu unapoteza muda wako kuhofu na kufikiria mabaya yatakayokuja badala ya kufikiri namna ya kukabiliana nayo.

Tumia nguvu zako, akili zako, hisia zako, katika kuwaza namna ya kuwa bora Zaidi, kutatua matatizo, na kuleta mabadiliko chanya. Kwa namna yeyote ile hofu, woga, kulia machozi, hakusababishi changamoto zikuonee huruma. Magumu yatazidi kuwa magumu kwasababu ulipoteza muda wako kufikiria ugumu badala ya njia za kutatua ugumu.

Unapokutana na tatizo tumia muda wako Zaidi katika kutafuta suluhisho na sio kulaumu, kuwa mwoga, kufikiri itakuaje.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading