HATUA YA 346: Unaweka Mchanganyiko Sahihi?

jacobmushi
2 Min Read

#Maji ni kimiminika ambacho kinatumika katika vitu vingi sana kwenye Maisha yetu. Ili uweze kuyatumia maji lazima uwe na lengo la kuyatumia la sivyo unaweza kuwa na maji na yasiwe na kazi.

#Maji ukichanganya na sabuni unapata povu la kufulia nguo. Maji hay ohayo ukiyachanganya na sukari na majani ya chai kisha ukayachemsha unapata chai.

#Maarifa unayopata hapa ni kama maji, unaweza kukuta wewe unayatumia maarifa haya kama maji ya kunywa pekee kumbe ungeweza kutafua michanganyiko ya aina nyingi katika Maisha yako na ukapata matokeo mbalimbali.

#Lazima ujue unataka nini ili uweze kujua ni aina gani ya maji unahitaji. Sio kila maji yatafaa kupikia, sio kila maji yatafaa kufulia, sio kila maji utayatumia kuoga labda kuwe na tatizo la maji.

#Kwenye Maisha kila unachojifunza ili kiweze kuleta matokeo unayotaka lazima ujue kuweka mchanganyiko sahihi. Huwezi kuchukua maji bila ya sabuni ukafikiri utaweza kufungua kwa ufanisi na ukapata matokeo mazuri.

#Maji ukichanganya na sukari pekee bila majani ya chai kisha kuchemsha huwezi kupata chai. Ni vyema ukajua ni mchakato wa namna gani unahitajika ili kupata yale matokeo unayotaka.

#Lazima ujue ni aina gani ya marafiki unahitaji. Lazima ujue ni nguvu kiasi gani unatakiwa kuweka ili lengo lako litimie. Lazima ujue ni rasilimali gani unahitaji kupata ili uweze kufanikisha lengo lako. Pasipo mchanganyiko sahihi lazima utaishia kwenye kushindwa.

#Kwasababu hakuna aliezaliwa anajua tunajifunza wakati tunafanya. Katika makossa tunayofanya ndio tunajua hapa palipaswa pafanyike namna hii. Huu mchanganyiko nilioweka haukuwa sahihi.

#Umezaliwa kuja kuleta njia mpya kwa yale yaliyoshindikana, endelea kujaribu hadi uweze kupata mchanganyiko sahihi ambao watu watautumia kama mfano na wao waweze kufanikiwa.

#Haijalishi umeshakosea mara ngapi endelea kujaribu, usikate tamaa wala kurudi nyuma. Kila unachojifunza nenda kaweke kwenye vitendo. Kuna mahali utafika milango itaanza kufunguka.

 

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
1 Comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading