Ukiona ugumu unazidi tambua ya kwamba ndio mwisho wa pambana unakaribia. Ukiona changamoto zinazidi kuwa nyingi basi ujue kuna sehemu unakaribia kuvuka.

Mbegu ikifukiwa chini baada ya muda huanza kuota wakati wa kuota sio wa mchezo. Ni mapambano kati ya mbegu inayojitoa kutoka kwenye maganda yake na kukutana na ardhi kwa juu. Lazima ikubali kusukuma ardhi ili iweze kuonekana duniani.

Endapo mbegu inapokutana na ardhi ingepoteza uwezo wake na kurudi chini kamwe tusiongeona tena. Vile vile wewe unapopitia changamoto ukiamua kukata tamaa ujue ndio unapotea kabisa. Ukiamua kuendelea kupambana lazima ushindi upatikane.

Wanaoshinda siku zote ni wale walioko kwenye uwanja wa vita. Waliopo nje wanaishia kuwa watazamaji pekee. Waliopo nje ya uwanja wa vita huishia kuwa washangiliaji wa wale walipo vitani.

Ndugu yangu acha kuendelea kutazama na kushangilia mapambano ya wenzako. Maisha yako ni uwanja wa vita. Unapaswa kupambana, unapaswa kupigana kisawasawa kile unachokitaka hakiwezi kuja hivihivi kama hujaweka nguvu kubwa.

Lazima ujikane binafsi kwamba ni lazima kile unachokitaka kitokee. Lazima ukubali kulipa gharama zote zinazohitajika. Kubali kuweka nguvu ya kutosha pale panapohitaji nguvu zako. Weka ujuzi wako wa kutosha pale panapohitaji ujuzi wako.

Usikubali kuwa mtu mwoga kwenye Maisha yako kwasababu upo vitani na woga hautakusaidia chochote, hakuna mshindi aliewahi kuwa mwoga. Mshindi yeyote ni jasiri na aliekubali kuzifuata changamoto hadi akazishinda.

Kumbuka vita inapokuwa ngumu ndio ushindi unakaribia hivyo usikate tamaa bali ongeza nguvu.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

2 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading