Mara nyingi tumekuwa tunafanya mambo kwasababu ya mifumo tuliyoikuta na kuambiwa ni sahihi lakini si kweli. Ukiwa shuleni mnapewa mtihani mmoja wanafunzi 100 na mnapimwa viwango vyenu vya mafanikio kwa mtihani mmoja. Lakini ukweli ni kwamba unaweza kupata sifuri kwenye mtihani lakini bado kuna jambo jingine unaweza kulifanya vizuri kuliko wale wenzako 99.
Inawezekana wewe umekuwa unapima mafanikio yako kwa kuangalia watu ambao mna umri mnaofanana. Ukiwatazama watu wenye umri kama wako unaona wameshapiga Hatua kubwa sana kwenye Maisha yao kuliko wewe. Ukiwatazama wale ambao ulisoma nao unaweza kukuta walishapiga Hatua sana kuliko wewe. Unaweza kufikiri kwamba wewe umeachwa kimafanikio, na uko nyuma sana.
Unaweza kupima mafanikio yako kwa kuwatazama wale watu ambao mnafanya vitu vinavyofanana. Ukiwatazama Hatua ambazo wameshafika unaweza kukata tamaa kabisa na kuona wewe unapoteza muda. Lakini mafanikio hayapaswi kupimwa kwa kuwatazama wengine wamefika wapi kuliko sisi au sisi tumewapitaje wengine.
Mafanikio yanapimwa kwa zile Hatua ambazo unapiga kila siku. Ukishakuwa na maono makubwa, ukaanza kuyafanyia kazi zile Hatua unazopiga kila siku ndio mafanikio yako. Kama jana uliweza kusoma kurasa 10 za vitabu leo ukaweza kusoma 20 basi leo umeongezeka. Pima mafanikio yako kwa kile ambacho unatakiwa kufanya.
Kile ambacho Mungu ameweka ndani yako ndio kinapaswa kuwa kipimo sahihi cha mafanikio yako. Jitazame kule unakotaka kufika miaka 10-20 ijayo kisha hakikisha kila siku unakuwa bora. Kama huwi bora basi huna mafanikio, kama huongezeki basi huna mafanikio. Mafanikio sio vile vitu ambavyo tayari unavyo tu bali ni yale maendeleo unayopata kila siku.
Mafanikio sio hatma sio sehemu ambayo unatakiwa kufika halafu ukatulia hapo hapana. Mafanikio ni vile vitu ambavyo unafanya kila siku na kuvifanikisha. Hakikisha kila siku kuna jambo unafanya na unaongezeka ubora.
Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog
Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/