HATUA YA 349: Umeshawahi Kukutana na Mtu wa Aina Hii?

Soma Vitabu Hivi;

MAFANIKIO KWENYE BIASHARA

SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO

USIISHIE NJIANI TIMIZA NDOTO YAKO.

MBINU 101 ZA MAFANIKIO

UMUHIMU WA MAONO.

Kuna aina mbalimbali za watu hapa duniani wenye kila aina ya tabia.

Kuna aina ya watu ambao ukikutana nao ukakaa nao dakika chache unapoteza mwelekeo kabisa wa Maisha yako. Watu hawa ni wale ambao mawazo yao siku zote ni kushindwa tu yaani hawana matumaini kwenye jambo lolote. Wao mara zote ni kulalamika, watailalamikia serikali, jamii, wazazi, elimu mbovu, hali ya hewa, jua, Mungu. Yaani kila kitu wanakilalamikia, mara nyingi watu hawa wanakuwa wamekata tamaa  kabisa kwenye Maisha yao wenyewe.

Kuna aina ya watu ambao ukikutana nao unapata nguvu mpya na unaanza kuona mwangaza kwenye Ndoto zako. Ukiwaelezea changamoto kidogo unayopitia watakupa mifano mingi ya watu waliopitia hapo ulipo na wakashinda. Ukikaa nao hawatakupa pesa bali watakuonyesha njia za kupata pesa, watakutambulisha kwa marafiki zao wakubwa ambao unaweza kuwauzia bidhaa zako na ukatengeneza kipato.

Ni jukumu lako wewe kuchagua ni aina gani ya mtu unampa nafasi kubwa Zaidi kwenye Maisha yako. Ukimpa nafasi yule ambaye anakunyonya nguvu zako basi ujue unapoteza muelekeo wa Ndoto zako. Ukimpa nafasi yule anakupa nguvu basi utaanza kukua kwa kasi kuelekea kwenye Ndoto zako kubwa.

Uzuri ni kwamba watu haw ani rahisi kuwatambua hasa kwa yale wanayoongea baada ya kukutana nao. Ukianza kuona mtu anasema hana pesa lakini muda wa kufuatilia mambo ambayo hayampi hata shilingi wala kumsaidia chochote ujue huyo atakupoteza.

Ukiona mtu haonekani kama ana pesa lakini anaweza kukwambia ukipata pesa yako usitumie yote weka akiba. Anaweza kukushauri kitabu kizuri cha kusoma ili uweze kupata mawazo mazuri ya biashara huyu ndio mtu wa kukaa nae.

KARIBU KWENYE EVENT YETU YA ONLINE HAPA https://jacobmushi.com/events/

Usikubali kabisa kupoteza Maisha yako na nguvu zako kwa watu wasio na mchango chanya kwenye Maisha yako bila kujalisha ni nani kwako. Wanaweza kuwa ndugu zako, marafiki zako wa zamani tangu utotoni, watu mnaosali pamoja, au hata wafanyakazi wenzako. Usiwape muda wako mwingi sana wala usikubali wakufahamu kwa undani maana watapata nafasi ya kukudharau.

Kama umesoma Kitabu kinaitwa Think and Grow Rich cha Napoleon Hill utaona kwamba kila kitu kinaanza kwenye fikra zetu na kama tutaweza kuziponya fikra zetu basi tutaanza kupata matokeo bora. Mojawapo ya vitu vinavyosababisha uwe bora kiakili ni watu ambao unashirikiana nao kila siku.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *