HATUA YA 35: Usitazame Nyuma.

Mara nyingi unapopitia magumu unatazama nyuma. Haijalishi ni ugumu kiasi gani unapitia sasa Usitazame Nyuma.

Endelea kusonga mbele ipo siku utatengeneza hadithi Nzuri ya kuwaambia watu.

Kuna msemo unasema au watu wengi hupenda kuutumia hasa wanakuwa wanatoa shuhuda zao. Msemo wa “tumetoka Mbali “

Ni mbali wapi utasema umetoka wakati unashindwa kuvumilia?

Ni hadithi gani utasema endapo ukitakiwa kueleza ulipotoka?

Kuna nyakati unapitia ili uje kutoa ushuhuda.

Usitazame Nyuma kwani mbele ndio ipo hatma yako.
Usikate tamaa tuendapo ni pazuri zaidi.
Usikate tamaa ndoto yako inakwenda kutimia.

Usikate tamaa ipiganie ndoto yako.  Lipo tumaini la kuchipuka kwa mti ulionyauka.

Napenda nikutie moyo kwamba mwisho wako ni Mzuri sana kama hutakata tamaa.

Karibu sana
Jacob Mushi
INUKA UANGAZE
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
Email: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

This entry was posted in HATUA ZA MAFANIKIO on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *