Mwanadamu siku zote hapendi aonekane anahusika na makossa yake mwenyewe. Na inapotokea amekosea au ameshindwa jambo Fulani anatafuta mtu wa kumbebesha yale makossa yake. Tangu mwanzo wa kuumbwa kwa dunia tunaona Adamu na Hawa walipopatikana na kosa la kula tunda la mti walioagizwa wasile kila mmoja alianza kutoa sababu za kwanini alifanya vile.

Adamu ambaye ndie aliepewa maagizo pamoja na majukumu yote yeye ndie aliwajibika kwa kiasi kikubwa kwa kosa lile. Alipoulizwa akaanza kujitetea na kutoa sababu kwamba mwanamke ndie aliempa tunda. Swala halikuwa ni nani kakupa tunda bali kwanini umeshindwa kufuata maagizo niliyokupa.

Katika Maisha yapo mengi yanatokea, inawezekana umepanda kufanya jambo ukashindwa, au ulitakiwa kuchukua Hatua Fulani. Ukiwa mtu wa kutoa sababu na kujitetea siku zote utaishia kukwama kwasababu hayo maelezo unayotoa hayabadilishi chochote.

“If you really want to do something, you’ll find a way. If you don’t, you’ll find an excuse.”

— Jim Rohn

Ukianza kuona mtu anatoa sababu nyingi za kwanini hajafanya jambo fulani, na kujitetea sana ujue kabisa mtu huyo hajataka kufanya. Kwasababu siku zote penye nia pana njia, pasipo na nia pana sababu nyingi na kujitetea.

Kujitetea hakuleti matokeo yeyote kwenye Ndoto yako.

Kutoa sababu hakukuletei pesa mikononi mwako.

Mtu yeyote anaeanza kuja na sababu kibao kwanini hajaweza kwanza namuona ni mtu anaekwepa majukumu yake mwenyewe. Ni ngumu sana kufanya kazi na mtu wa aina hii maana siku zote akiharibu hatakosa sababu ya kwanini ameharibu kazi.

Achana na sababu, na kujitetea wajibika pale unapokuwa umekosea, uzembe wako mwenyewe ukubali na chukua Hatua. Na kama hutaki kufanya jambo acha kujieleza sana wewe toa jibu moja fupi la hapana, haiwezekana. Kutoa sababu nyingi ni kupoteza muda tu.

Unapofanya jambo ukashindwa orodhesha makossa yako wewe mwenyewe kwanza kabla hujatupa lawama kwa mtu mwingine yeyote.

Usilaumu mtu yeyote.

Usilaumu serikali.

Usimlaumu shetani,

Usilaumu hali ya hewa,

Usilalamikie foleni ya magari.

Chukua Hatua pale unapotakiwa kuchukua Hatua, wajibika pale unapopaswa kuwajibika.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading