HATUA YA 352: Unachokikwepa Sasa Hivi…

jacobmushi
By jacobmushi
3 Min Read

Kiumbe hai chochote kina Hatua mbalimbali za ukuaji ambazo kinapitia hadi kufikia sehemu ambayo inakuwa ni ya ukomavu. Ili kiumbe hiki kije kuwa na mwisho mzuri lazima Hatua hizi zifuatwe kwa utaratibu. Huwezi kusema umepanda mahindi leo na ukayawekea mbolea na dawa le oleo ili yakue kwa haraka. Ukikimbilia kuyawekea mbolea mapema au ukayanyeshea maji mengi utayaharibu.

Katika Maisha ya mwanadamu  kuna Hatua mbalimbali za ukuaji, ukiachana na ukuaji wa mwili mwanadamu ana ukuaji wa akili na ufahamu. Na hapa ndio kunaamua wewe uwe mtu wa aina gani. Vile ambavo utavifanyia kazi mapema na kwa wakati wake ndio vitaamua wewe uje kuwa mtu wa aina gani.

Ni lazima kutambua kwamba chochote utakachojaribu kukikwepa sasa hivi kitakuja kutokea huko mbele na kinaweza kukuzuia tena. Changamoto unayoikwepa sasa hivi usipoitatua itakuja kukukwamisha siku moja katika Maisha yako.

Maisha yako huwezi ukamtegea mtu mwingine, chochote unachozembea lazima kije kukuletea shida huko baadae katika safari yako ya Maisha. Ukishindwa kuishi vizuri katika ujana wako lazima uje kuwa na uzee wa matatizo. Ukishindwa kutengeneza Maisha yako vizuri katika umri wa ujana lazima uje utumie nguvu kubwa sana unapokuwa mtu mzima.

Hakuna jukumu utakalolikwepa sasa likaondoka lazima kuna mahali litarudi na utatakiwa kulishughulikia na bahati mbaya sasa ni kwamba unaweza kutakiwa kulipa gharama mara mbili. Ukishindwa kutengeneza mifumo ya vipato kwa wakati uliopo mwenyewe basi ukija kuwa na familia kubwa ndio itakugharimu Zaidi katika kutafuta pesa.

Usije ukajidanganya kwamba kuna jambo limekwisha kwasababu umekunywa pombe ukalisahau. Usije ukafikiri unaweza kutoroka majukumu yako na wakati bado upo hapa duniani. Usije ukafikiri ukilalamika kwamba Maisha ni magumu au serikali inabana basi majukumu yako yataondoka. Bado utatakiwa kutatua na kutekeleza majukumu yako hata kama hali itakuwan ngumu kiasi gani.

Yatambue majira na nyakati za Maisha yako na uyafanye yale yanayokupasa kufanya ili usije kujitengenezea mzigo mkubwa huko mbeleni mwa Maisha yako. Yanayopaswa kufanyika sasa yafanye sasa. Kila jambo lina wakati wake, na endapo utalikwepa kwa wakati wake basi unaweza kuja kulipa gharama mara mbili wakati wa kulitekeleza jambo hilo.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading