HATUA YA 353: Uko Vile Ambavyo Unajiona.

jacobmushi
By jacobmushi
3 Min Read

Haijalishi sana watu wanasema au wanajua wewe ni nani kuliko vile ambavyo wewe binafsi ndani yako unavyoamini. Wapo wengi wanaweza kukusifia au kukuona hufai kama wewe binafsi utakuwa hujioni unafaa yote hayo hayatasaidia.

Unapaswa kutengeneza yule mtu ambaye unataka kuwa, andika vile ambavyo unajiona katika mtazamo chanya. Vile ambavyo ungejisikia vizuri Zaidi ukiwa hivyo. Imani mbaya ndani yetu zimeanza kujengwa tangu utotoni kutoka kwa watu ambao tuliwakuta wakati tunazaliwa.

Watu hawa kulingana na uzoefu wao hapa duniani wakatuingizia Imani zao ndani yetu. Watu hawa wengi wao wamekuwa ni watu walioshindwa Maisha, waliokata tamaa kabisa ya Maisha. Kile walichokuwa wanakiamini wakakiingiza ndani yetu.

Inawezekana uliambiwa ukoo wenu wote ni maskini yaani hakujawahi kutokea mtu mwenye mafanikio. Inawezekana uliambiwa kwenu hakunaga mtu anaolewa wote mnazalia nyumbani. Inawezekana uliambiwa kwenu hakuna aliewahi kufika chou kikuu yaani wote ni wajinga wajinga tu. Inawezekana uliambiwa kwenu kuna magonjwa ya ajabu yanayowapata mkifikisha umri Fulani.

Yote hayo yanaweza kuwa sababu ya aina ya Maisha ambayo unayo sasa. Mimi nataka nikwambie Imani zote ambazo ulijengewa zinaweza kuondoka kama utaamua kutengeneza Imani mpya. Imani hizi zinaweza kuwa kikwazo kikubwa kwenye Maisha yako kila unapoweka malengo makubwa inakujia kauli kwamba kwenu hamuwezagi. Kwenu wote walishindwaga hapa.

Anza sasa kutengeneza Imani mpya ndani yako. Imani ya kwamba inawezekana, ili Imani potofu ndani yako ziondoke lazima ujenge Imani mpya. Na hili halitachukua siku moja. Inaweza kuwa muda mrefu kidogo hadi utakapokuwa mtu mpya kabisa.

Andika vile ambavyo unataka kuwa katika wakati uliopo mfano “Mimi nina furaha sana, Ninafanikiwa kwenye biashara yangu, Ninaolewa, Ninaishia maisha bora, ninafaulu shuleni, ninatimiza malengo yangu, ninaendesha gari yangu” andika mambo yote yale ambayo huwa unaamini kwamba huwezi. Hakikisha unajisemesha maneno hayo asubuhi kabla hujaendelea na mambo mengine.

Kinachofata baada ya kuandika yale ambayo unataka kuwa au yale ambayo uliambiwa huwezi ni vitendo. Vitendo vingi ndio vitabadilisha na kuleta yale ambayo unayataka. Kama wewe ni mnene na unataka kupungua huwezi kupungua kwa kuandika kwenye notebook au kwa kujisemesha kwamba umekuwa na mwili mzuri. Unachopaswa kufanya ni mazoezi na kubadilisha mfumo wako wa ulaji wa chakula.

Vitendo pekee ndio vinavyoweza kumtoa mtu kutoka kwenye malengo aliyoandika hadi kuyafikia katika uhalisia wake.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading