Umeshawahi kujikuta unafanya kitu kimoja na hukimalizi kwasababu kila ukikitazama unakiona kama hakijakamilika bado?

Umeshakutana na hali ya kutaka kila kitu kiwe kiko sawa ndio uanze kuchukua Hatua?

Umepata wazo la kuanzisha biashara unaanza kuogopa “nikianza kabla sijaitengeneza vizuri sana ninaweza nikashindwa.” Au huu wimbo naona bado haujanivutia sana ngoja nirudi studio tena, au hichi kitabu naona kuna sehemu haijakaa sawa ngoja nikirekebishe tena.

Huu ni ugonjwa ambao unaweza kuwa sababu yaw ewe kuahirisha mambo yako. Kuna vitu vidogo vidogo unaweza kuvichukulia umakini sana kiasi kwamba ukajikuta huwezi kupiga Hatua.

Kubali kuanza hivyo hivyo na ikitokea umeshindwa utajifunza, ikitokea watu wamekukosoa basi utafanya vizuri Zaidi kazi inayofuata.hiyo kazi moja unayong’ang’ana nayo sana ili iwe bora inaweza hata isipendwe sana na wateja kama unavyofikiri.

Kwasababu una Ndoto kubwa ndani yako usitake kufanya kila kitu kionekane kama kwenye ile Ndoto yako kubwa. Wakati mwingine unakubali kufanya kitu cha kudharaulika ili kiweze kukubeba na kukupeleka sehemu ya maana Zaidi.

Chukua Hatua kwasababu muda haukusubiri wewe ukamilishe kila kitu. Unaweza kurekebisha kila wakati hadi ukaharibu. Kila siku ukiwatazama wengine wanaofanya kile uanchokifanya utaanza kuona cha kwako ni cha hovyo na utapata mawazo ya kubadilisha.

Usikubali ugonjwa huu uendelee kuwa kwako. Chukua Hatua, ikitokea hujafanya kwa ubora utajifunza. Sisiemi ufanye mambo ya hovyo ila fanya kwa uwezo wako wa mwisho na usiache kufanya kwasababu kuna kitu kimepungua kwako.

Haiwekani hata siku moja ukawa kamili, hata watu wakubwa sana kwenye unachokifanya bado wanakosea hivyo cha muhimu ni kufanya hadi pale uwezo wako ulipofikia na kutoa kazi yako kwa watu. Usisubiri hadi uone kila kitu kipo sawa, mawazo mengine yanakuja mbele kwa mbele.

Alieanzisha Amazon wakati anaanza hakuwa na wazo la kuuza bidhaa nyingine Zaidi ya vitabu. Cha kushangaza tunavyoongea sana karibu kila bidhaa inapatikana Amazon. Alieanzisha Facebook sidhani kama aliwaza watu watakuja kulipia matangazo yao ili yawafikie watu wengi, cha ajabu sana sasa hivi karibu kila mfanyabiashara anatangaza bidhaa yake na Facebook.

Wazo lako wakati linaanza haliwezi kuwa kamili. Chochote unachotaka kufanya hakiwezi kuwa kamili lazima kipitie Hatua za ukuaji ili kiweze kufikia kwenye ukamilifu. Anza kwa udogo ule ule ulionao, bila kujalisha utaonekanaje.

Cha muhimu sana ni wewe ujue kusudi lako na unapotaka kufika, hayo mengine yatajitengenezea njia kadiri unavyosonga mbele.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

Dakika 20 za Mafanikio https://jacobmushi.com/dakika20/

Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

One Response

Leave a Reply to Jacob MushiCancel reply

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading