HATUA YA 357: Watakukata Mbawa Zako.

Kuku na tai hawawezi kuishi pamoja na ili waweze kuishi pamoja njia ambayo ni rahisi sana ni tai kupunguziwa mabawa yake yanayomwezesha kuruka. Hii ni kwasababu kuku hata akijifunza vipi kuruka hataweza kwasababu mabawa yake hayamwezeshi yeye kuruka. Vilevile kuku hajaumbwa aweze kuruka hewani.

Kuna aina ya watu ambao ukiishi nao lazima ukubali kuwa kama wao. Huwezi kusema nitawabadilisha au nitawaambukiza hiki kilichopo ndani yangu. Hata ufanye vizuri kiasi gani bado watashindwa kukuelewa. Watu waliokata tamaa, na waliokubali aina ya Maisha waliyonayo. Watu ambao fikra zao zilishaharibiwa kabisa na hawawezi hata kidogo kuelewa lolote unalolifanya.

Usikubali kukatwa mbawa zako Rafiki kama wewe uliumbwa ili uruke. Usikubali kuishi Maisha ya chini kwasababu tu wale ambao upo nao watakukosa ukiwa mbali nao.

Watu ambao wanaweza  kukukata mbawa zako ni watu wanaolalamika. Watu wenye Imani kwamba serikali ndio inahusika na kuwajibika na ugumu wa Maisha yao. Watu ambao hawawezi kuona suluhisho kwenye matatizo na siku zote wanatafuta watu wa kuwabebesha lawama.

Watu ambao wamekata tamaa na Maisha yao wenyewe ukikaa nao kidogo wanakuambukiza kukata tamaa. Watu ambao hawaamini katika kufanikiwa wanatazama wingi watakumbukiza kile wanachokiamini.

Ni vizuri ukawa makini sana na yale ambayo unayasikia kutoka kwa watu kwasababu yana mchango mkubwa sana katika kukuharibu au kukutengeneza. Bahati mbaya matokeo hutayaona leo au kesho. Ukishapoteza dira ndipo utagundua kwamba ni yale maneno yalikuharibu.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

Dakika 20 za Mafanikio https://jacobmushi.com/dakika20/

Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

This entry was posted in HATUA ZA MAFANIKIO on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

1 thought on “HATUA YA 357: Watakukata Mbawa Zako.

  1. Jacob Mushi Post author

    “Imagine for yourself a character, a model personality, whose example you determine to follow, in private as well as in public.” -Epictetus

    Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *