Majani yanayojiotea yenyewe kwenye mashamba ambayo hayajapandwa kitu au hata yale yaliyopandwa mar azote huwa ni kwa ajili ya viumbe wengine ambao hawana uwezo wa kujitengenezea chakula chao binafsi. Hii ndio asili na ndio maana popote pale penye udongo mzuri ukipaacha bila ya kupanda chochote patatokea majani ya aina mbalimbali.
Wewe kama binadamu ni aina chache sana ya majani unaweza kuyatumia kama mboga, hii pia ni kwasababu wewe unapaswa kutafuta chakula chako mwenyewe na kwa bidii. Majani yote yayoota ni kwa ajili ya Wanyama wasioweza kujitengenezea chakula chao.
“Without hard work, nothing grows but weeds.” Gordon B. Hinckley
Hivyo basi twaweza kusema kwamba bila kufanya kazi kwa bidii hakuna chochote kitakachopatikana katika Maisha yako Zaidi ya magugu pekee. Kama hutofanya kazi kwa bidii chochote utakachokuwa unakipata hakitakuwa na thamani kubwa. Utaendelea kuishi kama watu wasio na uwezo wa kufanya makubwa. Utaendelea kupata magugu kwenye Maisha yako.
Maisha yako ni kama shamba ambalo unatakiwa ulifanyie kazi ili upate kile unachokitaka. Ukiliacha tu na kusubiri matokeo yaje yenyewe utaishia kukutana na majani ambayo hayafai hata kutumika kama mboga. Ukiona kuna mambo yanakuwa magumu maishani mwako ujue kwamba umeyafanya Maisha yako kama shamba ambalo limejaa magugu mengi sana ambayo huna kazi nayo.
Chochote unachokitaka kitokee maishani mwako, ili kitokee kunahitajika bidii sana.
“Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.”
Mithali 10:4
Kitabu cha mithali kinaweka wazi kwamba atendaye mambo kwa mkono wa ulegevu atakuwa maskini. Zao la uvivu ni umaskini, zao la bidii ni utajiri. Utakula matunda ya jasho lako. Ni lazima uweke bidii kwenye chochote unachokitaka hapa duniani. Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu;Bidii ndio itakufanya uweze kuwaza mawazo ya kitajiri na uweze pia kutimiza.
Rafiki Yako,
Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
Dakika 20 za Mafanikio https://jacobmushi.com/dakika20/
Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/