HATUA YA 359: Umeifahamu Malighafi Sahihi?.

By | July 4, 2018

Tumekuwa na watu ambao wanapenda vitu ambavyo vipo tayari tayari. Kila wanachokitaka wanataka kiwe tayari kimeshakamilika na wao waanze kutumia tu.

Ukweli ni kwamba tangu mwanzo tunaona asili ya vitu vingi ambavyo vinaonekana ni vichache ambavyo vimekuwa vimekamilika. Kila ambacho umekuwa unakitamani au unataka kukimiliki ni lazima ukubali kufuata mchakata wa kutengeneza.

Unataka mke/mume mwenye sifa nzuri lazima ukubali kumtengeneza, hawatokei wenyewe wakiwa wamekamilika. Lazima ukubali kwamba atakuja akiwa na mapungufu yake na ni kazi yakow ewe kuitengeneza ile bidhaa unayotaka kuiona.

Mungu anakupa wewe mti, lakini ukitaka meza unatumia mti kutengeneza meza, ukitaka karatasi unatumia mti kutengeneza. Sasa ili uweze kupata unachokitaka lazima ujue unahitaji malighafi ya aina gani ambayo itakuletea bidhaa unayoitaka.

Kujua unachokitaka haitoshi, ni vyema pia kujua ni aina gani inahitajika kukutengenezea bidhaa unayoitaka. Kama utashindwa kujua malighafi utaendelea kuumia kwa kutopata matokeo ya kile unachokitaka. Inawezekana wewe unataka karatasi lakini umepanda mahindi ukitegemea uvune mbao za karatasi. Umeshindwa kutambua kwamba mahindi yanatoa unga.

Kwa kupitia kujifunza ndio tunagundua hasa aina za malighafi ambazo zinahitajika kwenye vile vitu tunavyovitaka. Usiache kujifunza kwenye makossa ambayo unayafanya yatakusaidia uweze kugundua yale ambayo huyahitaji kwenye vile vitu ambavyo unavitaka.

Tunaposema kwamba hakuna formula ya mafanikio ambayo ukiitumia hiyo lazima ufanikiwe ni ukweli kwasababu kila mmoja ana kitu cha tofauti anachokitaka. Na kama ni hivyo basi kila mmoja atahitaji malighafi ya tofauti katika kutengeneza kile anachokitaka. Ni vizuri ukajua kwamba kuweza kwako wewe leo ndio unakuwa umetengeneza mwangaza kwa mtu mwingine anaekuja kesho.

Usiogope kujaribu hakuna mgunduzi aliegundua mambo makubwa pasipo kujaribu vitu vingi na njia mbalimbali. Kila unalofanya ukakosea basi umemsaidia mtu mwingine asije kurudia kosa hilo. Usiogope kukosea kwasababu kwa kukosea ndipo tunajua njia sahihi.

Tafuta malighafi sahihi, na hiyo ndio itakupeleka kwenye kujua njia sahihi ya kutengeneza kile ambacho unakitaka kwneye Maisha yako.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

Dakika 20 za Mafanikio https://jacobmushi.com/dakika20/

Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *