Katika Maisha kila siku kuna jambo kila mmoja anafanya kwa ajili ya kufanya Maisha yaende sawa.

Karibu kila kitu kinachofanywa kwenye dunia hii kinalenga katika kuyafanya Maisha yaw engine kuwa marahisi Zaidi.

Karibu kila biashara ipo kwa ajili ya kutatua matatizo ya wengine. Kabla hujawaza kuuza ili kutatua matatizo yako wewe mwenyewe unatakiwa ujue kwamba hakuna anaekuja kununua kwako kwasababu wewe una shida.
Hawanunui kwasababu wewe unataka upate ada ya kusomesha watoto. Hawanunui kwasababu ya kukufaidisha wewe.

Kila mmoja ananunua kwasababu ya shida zake mwenyewe. Ukilielewa hili litakusaidia sana ili ujue namna ya kumridhisha mteja wako na awalete wengine.

Najua unafanya biashara kwasababu ya malengo yako Fulani lakini hakuna mteja anaejali malengo yako mteja anakuja kwa ajili ya shida zake mwenyewe.

Kanuni ambayo itakusaidia ni wewe kumia muda mwingi Zaidi katika kulenga kutatua matatizo ya wateja wako kadiri ambavyo unawagusa ndivyo na wewe unakuwa umegusa shida zako.

Usitumie nguvu nyingi sana katika kutatua matatizo yako tumia nguvu nyingi kwenye kugusa matatizo ya watu wengine.


Ukitambua kwanini watu wanakuja kwako hapo ndipo utaweza kuendelea kuleta wengine Zaidi.

Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading