Tunaweza kutazama mti kwa pamoja lakini kila mmoja akauona kwa mtazamo wake wa tofauti. Kuna ambaye ataona mti kama mti tu, mwingine ataona kuni, mwingine ataona mbao, mwingine ataona matunda, mwingine ataona kivuli.

Kile kilichopo ndani yako na uhitaji wako ndio kinafanya uvione vitu katika namna ya tofauti na wengine. Hii ndio maana unaweza kuwapa watu wawili pesa kiwango kinachofanana na wakakaa sehemu zinafonana kila kitu lakini baada ya mwaka mmoja ukakuta kuna ambaye amerudi ile hali yake ya mwanzo na mwingine ana maendeleo makubwa.

Kutazama tunatazama kwa macho lakini kuona tunatumia akili. Unaweza kuwa na macho lakini huwezi kuona vitu sawasawa. Unaweza kuwa kipofu lakini unaona kuliko mtu mwenye macho. Wewe unaona nini katika dunia yako inayokuzunguka? Unajiona kama nani? Unayatazamaje mazingira na Maisha kwa ujumla?

Uwezo wako wa kuona vitu unasababishwa na vitu unavyoweka kwenye akili yako kila siku. Uwezo wako wa kutafsiri vitu unatokana na aina ya maarifa uliyonayo. Ukiwekeza kwenye maarifa na kwenye akili yako huwezi kuwa maskini, hii ni kwasababu utaweza kuona fursa hata ile sehemu ambayo kila mtu amekata tamaa kabisa.

Ukiweza kuwa na mtazamo wa tofauti unakuwa mleta majibu kwa wengine. Uwezo wa mtu kuona vitu kwa usahihi ni ukubwa wake wa macho ya ndani. Macho ya ndani yanakuzwa kwa kuwa na maarifa ya kutosha kwenye akili yako. Wakati wengine wanaona mti katika mtazamo mmoja wewe unaweza kuwaonyesha namna ya kuutumia mti mmoja kuotesha miti mingi Zaidi huku ukiutumia ule mmoja uliobakia kwenye vitu vingi zaidi.

Wakati wengine wanawaza na kuona kutumia wewe mwenye macho ya ndani yenye uwezo mkubwa utaona namna ya kuzalisha ili wao watumie. Chochote kile kinachoendelea kwenye Maisha yako ni mazao ya fikra zako. Na ndio maana tunasema ukibadili fikra zako unakuwa umebadili Maisha yako.

Badili mtazamo wako, soma vitabu, jichanganye na watu wenye uwezo mkubwa kuliko wewe ili uweze kuona wanavyoona.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

Dakika 20 za Mafanikio https://jacobmushi.com/dakika20/

Huduma Zetu https://jacobmushi.com/huduma/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading