Katika Maisha yako usikubali kuwa mtumwa wa kufanya vitu ili watu wakuamini au wakuthamini au wakukubali. Chochote kile unachokifanya sababu ya kwanza inatakiwa kuwa ni moyo wako uwe unapata furaha, sababu ya pili iwe ni kuna Maisha ya mtu unayasababisha yawe bora.

Haya mengine yote ambayo yanakuja huku Njiani kama kusifiwa, kujulikana sana, kupongezwa, kupewa tuzo, na mengine mengi hayatakiwi kuwa sababu kuu ya wewe kufanya hicho unachokifanya. Haya mara nyingi hayadumu na wala hayaletwi furaha ya kudumu.

Wachungaji, Wahubiri, na Viongozi wa Imani mbalimbali huwaambia wale waumini wao kwamba kuna pepo nzuri baada ya kifo. Wengine tunaambiwa kuna mbingu, paradiso na mengine mengi. Sasa kuamini hayo yote ni suala la mtu binafsi. Haulazimishwi kuamini, ila kinachokufanya uwe mfuasi ni kwasababu una amini. Nataka kusema hivi kwenye kile unachokifanya usipoteze muda kuwaaminisha watu juu ya Ndoto yako kubwa uliyonayo hasa wale ambao hataki kuamini.

Una jukumu moja kubwa sana la kufanya ambalo ni kuendelea kufanya kila siku kile ambacho unakiamini na unataka kije kilete matokeo. Kuna watu siku zote watakupinga hata ukifanikiwa, watasema ulisaidiwa au uliiba na mengine mengi ya ajabu.

Yeyote anaekwambia unachokifanya unapoteza muda yeye ndie anapoteza muda kukufuatilia wewe badala ya kufanya yake. Kama anaona unapoteza muda vyema yeye akaenda kufanya anachoona sio cha kupoteza muda halafu matokeo yenu ndio yapingane.

Usiwapinge kwa maneno acha matokeo ya kile unachokifanya ndio yaje yapinge maneno yao. Ukiongea utachoka, tumia nguvu zako na muda wako kufanya yale ya muhimu kwenye Maisha yako. Kile kinacholeta furaha ndani yako na kinachogusa wengine hicho ndio cha muhimu kwenye Maisha yako.

Hata ukifika mbinguni ukarudi watasema tutaaminije kama umefika kweli?

 

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

Jiunge na Usiishie Njiani Academy Hapa https://jacobmushi.com/academy/

Huduma Zetu https://jacobmushi.com/huduma/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading