HATUA YA 366: Hakuna Hali Yeyote Inayodumu Kwenye Maisha Yako.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Maisha ni muunganiko wa matukio ya aina mbalimbali ambayo yanaendelea kila siku. Kuna nyakati utakuwa na furaha sana na kila unalolifanya linaleta matokeo yale uliyokuwa unayataka. Kuna nyakati mambo yatakuwa ni mabaya changamoto nyingi na utatakiwa uwe unawaza sana. Unachotakiwa kutambua ni kwamba yote hayo ndio Maisha.

Haujawahi kuambiwa kwamba Maisha yatakuwa ni marahisi na kufurahi tu siku zote. Kama umeshaelewa hivyo cha muhimu ni kutokujisahau katika hali yeyote ile. Ukipitia magumu sana usisahau kwamba yatapita, ukipitia hali za furaha na kufurahisha sana usijisahau kwamba hiyo hali haitadumu milele.

“Remember, no human condition is ever permanent. Then you will not be overjoyed in good fortune, nor too sorrowful in misfortune.”
― Socrates

Chochote unachopitia tambua ya kwamba hakitadumu siku zote, cha muhimu ni wewe kujua unafaidi vipi hali unayoipitia ili ikishaondoka usije sema ningejua. Kuna hali zinakuja kwenye Maisha yetu na tukishindwa kuzifurahia au kuzitumia vyema zikiondoka hazirudi tena. Ni vizuri ukajiweka katika namna ya kuweza kufaidi kila hali ambayo unaipitia. Iwe hali ngumu itumie kama somo, ikiwa ni hali nzuri ya kufurahia basi pia hakikisha unaitumia vyema ili usije kujutia na kusema ningejua.

Usilie sana ukasahau kwamba sio wewe unapitia hali hiyo mbaya. Usihuzunike sana na kufikia kumkufuru Mungu wako kwasababu yam abaya ambayo unapitia. Tambua ya kwamba hayatadumu milele. Pia jifunze kuyatumia magumu hayo kwa faida, badala ya kulalamika na kulaumu, kukaa wakati wote una huzuni yatazame yale mazuri ambayo unayo. Una uhai, na uhai ni ishara ya kwamba kuna mazuri mengi yanakuja kwa aiili yako kesho.

Usijisahau kwenye yale mazuri ambayo yapo kwako siku zote na ukaanza kuwaumiza wasio nacho. Hakikisha kila ulichobarikiwa unakitumia kuwabariki wengine na sio kuwaumiza, kama nilivyokwambia sio kila hali itadumu maishani mwako hivyo huijui kesho yako itakuaje. Usitumie chochote ambacho unacho kuwaumiza wengine.

Maisha yako ni zawadi kwa ajili ya wengine. Hakikisha kila siku kuna mwanadamu mwenzako anafurahia uwepo wako hapa duniani.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

Jiunge na Usiishie Njiani Academy Hapa https://jacobmushi.com/academy/

Huduma Zetu https://jacobmushi.com/huduma/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading