HATUA YA 367: Kama Sio Sahihi Usifanye na kama Sio Kweli Usiseme.

Jambo lolote unalotaka kufanya lazima uwe na muda wa kujiuliza faida na hasara ya jambo lenyewe katika Maisha yako na ya wengine. Karibu kila jambo ambalo utafanya leo liwe baya au zuri linagusa Maisha ya wengine inawezekana ni moja kwa moja au sio moja kwa moja.

Kwa kupitia matendo yako kuna Maisha ya wengi unayagusa, kwa kupitia maneno yako kuna Maisha ya wengi pia unayagusa.  Unaweza kuonesha vitendo vibaya mbele ya mtu mmoja lakini ukawa umewaharibu watu mia walioko nyuma yake.

Unaweza kuongea maneno mabovu mbele ya mtoto ambaye anatakiwa kuja kuwa mtu mkuu sana. Na kwa maneno yako mabaya ukawa umeathiri watu wengi sana.

Kabla hujachukua Hatua kufanya kitu jiulize kina faida gani kwako na kwa wengine. Kama neon halijatoka mdomoni mwako jiulize ungekuwa unaambiwa wewe lingekusaidia?

“If it is not right do not do it; if it is not true do not say it.”
― Marcus Aurelius, Meditations

Kama jambo sio sahihi usilifanye, na vile vile kama jambo sio la ukweli usiliseme. Unaweza kusikia maneno mengi mazuri na mabaya juu ya watu kabla hujaanza kuyasambaza jiulize maswali.

Je ni kweli?

Kama ni kweli maneno haya yana manufaa gani kwa watu wakiyajua?

Kama ukiona hakuna manufaa yeyote basi achana nayo mara moja. Ni kweli inawezekana mtu amefanya jambo baya kabisa. Huo ukweli haukupi wewe ruhusa ya kusema kwa wengine lazima ujiulize ukisema utakuwa umemsadia mtu au umemchafua.

Inawezekana umesikia jambo lolote baya juu ya mtu ukafuatilia na ukathibitisha kwamba ni kweli. Jambo jema au Hatua bora ya kuchukua ni ile ambayo itamsadia mlengwa. Kusambaza uovu wa mtu kila mahali hakusaidii kitu chochote. Kwanza kunaonesha wewe ulivyo mtu mbaya usieweza kukaa na mambo ya watu.

Kama jambo halileti faida kwako au kwa wengine liache.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

Jiunge na Usiishie Njiani Academy Hapa https://jacobmushi.com/academy/

Huduma Zetu https://jacobmushi.com/huduma/

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading