Mtoto mdogo ndio binadamu pekee ambaye kile anachokifanya unaweza kuamini anakimaanisha kabisa. Hii ni kwasababu mtoto anakuwa hajajua chochote juu ya ukweli wala uongo, hajui kudanganya wala kuficha kitu.
Mtoto mdogo ana Maisha yasiyo na hila ndani yake, anaishi kwa uhuru mkubwa kuliko binadamu wengine ambao tayari tumeshaingiza chachu ndani yetu. Kiwango hiki ndio kiwango cha juu sana cha mafanikio ya mtu mzima, endapo Maisha yako hayatakuwa kama ya mtoto mdogo basi ni kwamba unaishi kwa mateso.
“Give me beauty in the inward soul; may the outward and the inward man be at one.”
― Socrates
Mwanafalsafa Socrates anasema, Nipe uzuri wa ndani (nafsi), na mtu wa ndani na wa nje awe ni mmoja. Yaani kwamba yale Maisha ambayo unayaishi ya nje yasiwe ni maigizo bali yawe ndio kweli ndani yako. Wengi kwa nje tunaonesha furaha lakini ndani tuna huzuni kubwa. Wengi ndani yetu kumejificha mambo makubwa sana na mengine yamekuwa ni mateso makubwa ambayo tunatembea nayo.
Kama wewe ni katili basi kuwa katili usijifiche na kuonesha wewe ni mwema. Kama wewe ni mchoyo onesha wazi uchoyo wako usijifiche. Kama wewe ni mwema basi tenda wema onesha wema kila mahali. Kama una upendo onesha upendo, kama una furaha ishi kwa furaha.
Luka 18:17- Nawaambieni kweli, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hataingia katika ufalme huo.”
Maisha yam toto mdogo ndio kipimo cha Maisha ya uadilifu na usafi wa Maisha ya mtu. Ni kweli watoto hwafikirii kama sisi watu wazima lakini haina maana kwamba kufikiri kukupeleke kutenda yaliyo maovu. Maisha yako kama yanaweza kuendana na namna watoto wanavyoishi hicho ndio kipimo halisi cha ubora wa Maisha yako.
Mtoto mdogo akiumizwa atalia kwa muda mchache na atasahau, akichapwa na mzazi atalia lakini baada ya muda lazima arudi kwa mzazi wake. Sisi watu wazima tumekuwa watu wa vinyongo na chuki kwa wale ambao wanatukaripia na kutuonya. Tumeyaweka mioyoni mwetu yale ambayo watu wametutendea.
Ukweli ni kwamba tulizaliwa tuishi Maisha kama yam toto mdogo, na ninaposema haya nazungumzia ule moyo wa mtoto mdogo ulivyo ndani ndio mioyo yetu ilitakiwa iwe hivyo. Nina amini inawezekana, unaweza kutengeneza upya ndani yako.
Anza taratibu.
Samehe
Tenda wema
Usiwe Msemaji wa Mabaya ya Wengie kwa Wengine.
Ishi vile Moyo Wako Unapenda.
Rafiki Yako,
Jacob Mushi