Hakuna kitu kibaya sana ambacho kinawafanya watu washindwe kwenda mbele kama historia mbaya ya Maisha yao. Mfano wewe kwenu tangu umezaliwa umekuwa unaimbiwa wimbo wa sisi ni maskini, kwetu hawajasomaga hata mmoja, kwetu hakuna mtu mwenye akili. Maisha yako yote yanakuwa yakiifuata ile historia ambayo umekuwa unaambiwa.

Inawezekana umeshindwa kufanya vizuri kwenye vitu vingi maishani kwasababu uliambiwa kwamba kwenu wana historia mbaya. Lipo neno moja la baraka juu yako leo. Unakwenda kuleta utofauti kwenye Maisha yako. Amua leo kuwa mtu wa tofauti na ubadili historia ambayo umekuwa unaambiwa kila wakati.

Haijalishi jana ulikosea wapi, haijalishi umekuwa na historia ya aina gani ya Maisha. Kitu pekee ambacho kitakufanya uweze kufika mbali ni kuangalia kilichopo mbele na sio ambacho kipo nyuma yako.

Ukitaka kukimbia kilichopo nyuma yako unatakiwa uanze kukimbilia kilichopo mbele yako. Ukibaki unatazama kile ambacho kipo nyuma utashindwa kufika kule mbele. Njia rahisi ni kuachana na historia yako mbaya kwasababu huwezi kubadili na ukimbilie hatma ya Maisha yako.

Thubutu na chukua Hatua katika kufanyia kazi Ndoto zako. Kila kitu ambacho umeweza kukifikiria basi kitu hicho kinawezekana.  Na kama kuna wengine wengi wameweza basi hata wewe pia unaweza.

Kama utaweza kuanza kuchukua Hatua leo basi utaanza kuwa mbali kabisa na zile historia mbaya za Maisha yako. Ukianza kuchukua Hatua kuelekea kwenye Ndoto zako moja kwa moja unakuwa unaanza kuiacha kwa mbali ile historia mbaya ya Maisha yako.

Usikate tamaa, usiangalie kile ambacho huna tazama vile ambavyo tayari unavyo na uanze kuchukua Hatua.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading