Umewahi kuwa na wazo lako zuri sana ambalo linakuhamasisha mno ukakutana na mtu mmoja ukamuelezea na kwa sentensi yake moja aliyokujibu ikakufanya ukaliharibu kabisa wazo lako? Hii imewahi kunitokea mimi sio mara moja ila baada ya mud asana nikajifunza kwamba kila mtu anaona kwa namna yake ya tofauti.

Nikajifunza kwamba kabla hujafanyia kazi maoni ya wengine hakikisha kwamba umeyachambua vizuri yasije yakabadili yale maono yako kwenye kile ambacho ulikuwa unataka kufanya.

Ninachotaka kukwambia usikubali kamwe maoni ya mtu mmoja yaharibu kile kitu kikubwa ambacho umekuwa unataka kufanya. Watu wengi wameacha mawazo yao mazuri sana na ambayo yangebadilisha Maisha yao kwasababu ya mtu mmoja tu ambaye alikuwa anamuamini sana alimwambia hili wazo lako haliwezekani.

Usikubali wala kuridhishwa na mtu mmoja kwa neno lake alilosema, hakikisha wewe ndio umefanya maamuzi sahihi kabla hujafikia mwisho.

Siku zote penda kukumbuka ni kwanini ulitaka kufanya kile ambacho unakifanya kabla hujakata tamaa kwa yale ambayo umekutana nayo njiani.

Usikubali maoni ya mtu mmoja yaharibu siku yako.

Usikubali kuishia njiani kwenye wazo lako kwasababu ya maoni ya mtu mmoja.

Usikubali kupoteza mwelekeo wa kule unapoelekea kwa maoni ya mtu mmoja.

Usikubali kuliacha kusudi lile lililoamua wewe kufanya jambo kwasababu ya maoni ya mtu mmoja.

Kuna watu watakuja na maoni yao ili kukupima kama kweli unakiamini kile unachokisema na ukishatetereka basi inaonekana huwezi kusimamia kile unachokiamini.

Mtu anaweza kuja na maoni mazuri sana lakini Kumbe yale maoni sio ya wakati huo lazima ujue ni yapi ya kufanyia kazi sasa na yapi ni ya Baadae. Usikubali kuyumba na kupoteza mwelekeo kwasababu ya maoni ya mtu mmoja. Jiamini wewe amini ile nguvu iliyokusuma kuchukua Hatua na hakikisha unafikia ule mwisho ambao ulikuwa unauona ndani yako.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

https://jacobmushi.com/huduma/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading