Muda wa asubuhi ndio wakati ambapo akili yako inakuwa na uwezo Mkubwa sana wa kufikiri na kufanya maamuzi magumu. Kama ukiweza kuutumia muda huu vizuri kufanya yale ya muhimu kwenye Maisha yako utakuwa na maendeleo makubwa sana.

Watu wengi wanapoamka asubuhi kitu cha kwanza kufanya ni kushika simu zao kuangalia ni nani amewapigia au kuwatumia sms. Hii ni hatari sana kwasababu mambo hayo hayaleti mchango wowote chanya kwenye siku yako.

Watu wengi wakiamka asubuhi wanatembelea mitandao ya kijamii kutazama kilichojiri kuangalia matukio mbalimbali ambayo hayawasaidii chochote na wala hawaendi kuyafanyia kazi siku hiyo.

Kama wewe ni mmoja wa watu wa aina hiyo maana yake utakuwa kila siku unalalamika mambo yako hayaendi Kumbe wewe ndio kisababishi kikubwa. Unapoamka asubuhi hupaswi kabisa kushika simu yako.

Ukianza siku yako kwa kulalamika utaimaliza kwa kulalamika. Ukianza siku yako kwa kufuatilia matukio utaishia kufuatilia matukio. Kama wewe sio mtangazaji au Mwandishi wa Habari matukio yanayoendelea hayakuhusu sana labda yawe yanagusa familia yako.

Tumia muda wako vizuri kwasababu ndio kitu pekee ambacho kikipotea hakirudi tena. Huwezi kurudisha tena muda nyuma. Sio kila simu lazima upokee asubuhi, sio kila ujumbe uliotumia lazima uusome asubuhi. Unaweza kupokea simu au kusoma ujumbe ukakuta siku yako ndio imeharibika kabisa. Fanya yale ya muhimu ambayo nimekueleza kwenye aya inayofuata.

Unapoamka asubuhi unapaswa kuanza kuyatazama malengo yako, mipango yako ya siku hiyo, pitia yale mambo ambayo unapaswa kufanya siku hiyo. Unatakiwa usome kitabu angalau kurasa kumi na kuendelea, unatakiwa uongeze kitu chanya kwenye akili yako na sio takataka zozote ambazo hazikusaidii chochote.

Nimekuandalia Kozi inaitwa DAKIKA 20 ZA MAFANIKIO. Kozi hii imebeba mambo 3 ya muhimu sana ambayo kila mmmoja anaeyataka mafanikio anapaswa kuyafanya kila siku asubuhi hadi yawe tabia zake kabisa. Mambo haya huwezi kuyafanya mwenyewe unahitaji kiongozi wa kukufuatilia, mimi nimejitolea hilo. Karibu kwenye kozi hii ya pekee sana uweze kufika viwango vya juu sana.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

https://jacobmushi.com/huduma/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading