Usipoteze muda wako hata kidogo kufuatilia Maisha ya mtu ambaye wewe binafsi huna mpango wa kufika pale alipo. Itakuwa ni sawa na mtu anaetaka kupungua lakini hajui ni vyakula gani hasa anatakiwa ale ili asiendelee kuongezeka unene.

Lazima ujue ni vitu gani ulishe ubongo wako, na huwezi kujua vizuri kama huna mahali unataka kufika. Tafuta mtu mmoja au hadi watatu ambao utajifunza kwenye Maisha yao. Yapo mengi ambayo utaona yanafaa  kufanyia kazi kwenye Maisha yako na matokeo yake utaanza kuyaona.

Kila mtu kulingana na kile ambacho amezaliwa kufanya kuna mtu mmoja au Zaidi ambaye ameshafanikiwa kwenye kitu hicho. Hivyo basi ni muhimu ukajua huyo ambaye amefanikiwa sana kwenye kile unachotaka kufanya na ukafuatilia vizuri njia gani alitumia hadi akafika pale alipo.

Kitu cha muhimu ni kujua yale mambo anayofanya kila siku ili kumfanya aendelee kubakia kwenye mafanikio. Zipo tabia za muhimu ambazo ukizijua utafahamu ni kipi ufanye ili uweze kufika kwenye kiwango ambacho unataka wewe.

Hakikisha unajua wanaamka saa ngapi, wanafanya nini wanapoamka, wanasoma Vitabu gani. Walikosea wapi ili wewe usipite pale pale walipokosea tena. Tafuta kujua ni vitu gani wanavifanya na vinaleta matokeo mazuri na wewe uvifanye sawasawa.

Rafiki yangu sio kwamba nakutania ukiweza kujua wale waliofanikiwa wanafanya vitu gani, wanasoma Vitabu gani, na wewe ukaenda kufanya sawasawa na wao lazima utaanza kupiga Hatua kuelekea kwenye mafanikio makubwa.

Yapo mambo mengi ambayo unaogopa kuyafanya ukiyajua waliofanikiwa walifanyaje woga utakutoka na utaweza kujaribu bila ya wasiwasi.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading