As Confucius said: Everything has its beauty, but not everyone sees it.

Confucius alikuwa ni mwanafalsafa wa Kichina aliwahi kusema kwamba kila kitu kina uzuri wake lakini sio kila mtu anaweza kuona uzuri kwenye kila kitu. Na huu ndio ukweli hata kama mtu ni mbaya kwa kiasi gani bado kuna sehemu atakuwa mtu mzuri.

Unaweza kumuona mtu ni mbaya kwako kulingana na sehemu uliyopo wewe au ile sehemu ambayo unatumia kumtazama lakini bado mtu huyu akiridu nyumbani ataonekana mzazi mzuri kwa watoto wake.

Kama umeweza kuona mabaya ya mtu yatumie kujirekebisha na sio kuyasema kwa wengine. Hii ni kwasababu hata wewe kuna mahali watu wanaweza kuwa na tafsiri mbaya juu yako kulingana na sehemu ambayo upo.

Unaweza kumuona askari ni mtu mbaya sana kwasababu upo mahabusu lakini askari huyo huyo kuna watoto wanamshukuru Mungu kwa ajili yake kwa kuweza kuwasomesha, kuwalisha na Maisha yanaenda vizuri nyumbani.

Usikubali  ubaya wa mtu ubaki ndani ya moyo wako unatakiwa ujifunze kumuacha mtu na mabaya yake kama huna uwezo wa kumrekebisha. Kitu kibaya sana ambacho watu wanafanya ni kuona mabaya ya mtu na kuondoka nayo.

Unaona mtu amefanya mabaya hujaweza kumsemesha ujue ni kwasababu gani amejikutana anafanya hivyo unamjadili siku nzima na mwisho wa siku wewe unakuwa mtu mbaya Zaidi yake kwasababu umetumika kueneza ubaya wa mtu.

Napenda Rafiki yangu wewe usiwe mtu wa aina hii ambaye anaona mabaya peke yake kwa watu. Hakuna mtu mbaya peke yake na mtu mzuri pekee yake. Kuna mtu kwako anaweza kuwa mzuri lakini akienda sehemu nyingine anaonekana ni mtu mbaya sana.

Unachotakiwa kuelewa ni kwamba kila mtu ana sehemu tofauti tofauti anavyoeleweka kulingana na aina ya Maisha ambayo ameishi. Usikubali kubaki na ubaya wa mtu moyoni mwako.

Ona mazuri kwa watu na watu watayaona mazuri ndani yako.

Rafiki Yako

Jacob Mushi

https://jacobmushi.com/huduma/

3 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading