HATUA YA 382: Njia Pekee ya Kuiponya Dunia Hii.

Pamoja na matukio maovu ambayo yanaendelea kila siku hapa duniani, tunasikia watu wanauwawa kinyama, wengine wanafanyiwa Matendo mabaya sana kama ubakaji, na mengine unayoyafahamu ipo njia moja ambayo kila mmoja akiweza kuifanya anaweza kuiponya dunia.

Pamoja na kuwa mambo haya yanaumiza sana kiasi kwamba unaweza kuwaza kufanya mambo mabaya sana lakini hiyo haitasaidia maana ukifanya mabaya kwao hutakuwa tofauti na wao.

Njia pekee unayoweza kuitumia kuwasaidia wengi ni kuendelea kueneza upendo na kutendeana wema. Watu wakifahamu juu ya upendo wakapendana lazima wataacha uovu.

Chanzo cha maovu mengi tuyaonayo duniani ni chuki, visasi na ubinafsi. Mtu anaamua kuwa mbaya tu ili aitetee nafasi aliyonayo. Mwingine anakuwa mbaya kwasababu alitendewa ubaya na wengine. Mwingine anakuwa mbaya kwasababu alijengewa ubaya ndani yake.

Huwezi kuwaondoa wabaya kwa kuwaua kwasababu wakati wewe unawaua unakuwa unatengeneza wabaya wengine Zaidi. Katika wale waovu kuna watoto wao ambao huenda walikuwa wanawapenda baba zao sana na hawakutambua kama ni waovu sasa wewe kitendo cha kumuondoa muovu unakuwa umetengeneza muovu mwingine.

Ukiweza kumponya mtu mwenye chuki kwa kumuingizia upendo utakuwa umewaponya wengi. Ukiweza kumponya mtu mwenye ubinafsi kwa kumfanya awe mwema kwa wengine na awafikirie wengine utakuwa umewaponya wengi sana.

Njia pekee ya kuondoa uovu hapa duniani ni sisi ambao kuendelea kupanda mbegu njema kwa kasi sana kuliko mtu mwingine yeyote. Mbegu njema zikiwa Nyingi kila mahali zitaota kwa kasi na kuzipoteza mbegu za uasi zilizojaa ndani ya mioyo ya wengi.

Hii ndio njia rahisi tunayoweza kuitumia kila mmoja na kila mahali.
Hakikisha unakuwa balozi wa Amani na upendo.
Usisambaze Chuki, waambie watu wapendane hii ndio ya kukomesha visasi na mambo mabaya yanayoendelea duniani.

Mimi Nimeamua kuanzia leo nitakuwa Balozi wa Amani na Upendo

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading