Maisha magumu uliyonayo sasa, madeni sugu, Kipato cha chini na matatizo mengine yote uliyonayo kuna mtu mmoja pekee anahusika kuyatatua. Ukweli unatakiwa umfahamu mtu huyu ili uweze kukaa nae vizuri sana akuwezeshe kuondokana na shida ulizonazo.


Kwenye Makala yetu ya leo utakwenda kumjua mtu huyu ambaye anahusika kabisa na ni jukumu lake kukufanya wewe ufikie mafanikio. Maisha yako yatakuwa magumu sana kama hujamjua mtu huyu, utaendelea kubaki hapo ulipo kama hujamjua mtu huyu.


Utaendelea kulalamika kila siku kwasababu hujamjua mtu huyu. Utaendelea kuwatupia lawama wazazi na watu wengine mbalimbali kwasababu hawajakusaidia vitu Fulani lakini unasahau mtu huyu ndiye anahusika.

Nataka kukwambia mtu huyu ni nani lakini kabla sijakuonyesha mtu huyu nataka nikwambie sasa Maisha yako yanakwenda kubadilika baada ya kumfahamu mtu huyu. Kwasababu mtu huyu ndie unatakiwa umbebeshe majukumu yako yote. Mtu huyu ndie anatakiwa akupe suluhisho la matatizo yako yote uliyonayo. Hivyo basi kwakuwa nakwenda kukuonyesha mhusika mkuu wa kutatua matatizo yako naomba ujiandae na ujisikie vizuri.

Mtu huyu ni wewe!

Najua utakuwa umeshangaa sana lakini mtu pekee anaehusika na hayo yotee niliyoyataja ni wewe. Anaehusika kuyafanya Maisha yako yafanikiwe sio mtu mwingine ni wewe. Mimi ni kweli kabisa natamani sana nione unafanikiwa kwenye kile unachokifanya lakini kama hujaamua kutoka ndani ya moyo wakoa huwezi kupata mafanikio yeyote.

Amua leo kuchukua majukumu yote ya Maisha yako na uanze kuwajibika ili ndoto zako zitimie. Hakuna mtu mwingine atakuja kuwajibika kwa ajili yako.
You must take personal responsibility. You cannot change the circumstances, the seasons, or the
wind, but you can change yourself.
JIM ROHN
Jim Rohn anasema inakupasa uchukue majukumu yako, huwezi kubadili mazingira, au msimu au upepo lakini unaweza kujibadilisha wewe mwenyewe.

Hivyo mtu pekee anaehusika kubadili Maisha yako ni wewe mwenyewe. Acha kutafuta mchawi wewe ndiye umejiloga. Anza kutafuta dawa ya kujitibu.

Kama umefikia kusoma Makala hii halafu bado hujabeba majukumu yako yote mwenyewe unatakiwa uanze kuchukua hatua. Hakuna namna nyingine. Maisha yako yataanza kubadilika pale tu utakapobeba majukumu yote yako peke yako. Pale ambapo kila linalotokea kwenye Maisha yako wewe pekee ndie unatakiwa utafute suluhisho.

Karibu sana.
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading