Imekuwa ni kawaida kusikia watu wanalalamika wameumizwa kihisia, na wanasema hawatakaa wapende tena. Imekuwa ni kawaida pia kuona watu wakilalamikia mambo mbalimbali ambayo walijitoa sana na kisha yakaja kuwaumiza kuliko walivyotarajia.
Unachotakiwa kujifunza hapa ni wewe binafsi kujitahidi uweze kudhibiti hisia zako. Usipende kuziachia zikatoka au zikaonekana san ahata kwa mtu ambaye bado hujajua kama ana mpango gani na wewe. Ni sawa na kutoa maji kwenye ndoo na kutaka yaingie yote kwenye kikombe lazima utayamwaga. Unapozitoa hisia zako kwa mtu ambaye bado hajafungua moyo wake kwako lazima utaumizwa kwasababu hisia zako zinakuwa zinapotea hewani.
Jifunze kudhibiti hisia zako, hasa kama umeshajijua kuwa wewe ni mwepesi wa kupenda mtu. Usipende kuonesha waziwazi ule udhaifu wako kwa watu ambao hujawajua vizuri kwasababu wengine watautumia kukuumiza.
Hivi umeshawahi kujiuliza kwamba kama kuna mtu ambaye hapendi kupendwa? Mbona sasa unakutana na mtu anasema nilimpenda sana lakini akaniumiza? Ukweli ulimpenda ila yeye hakuona upendo aliona udhaifu wako.
Usitumie muda mwingi sana kuwaza Zaidi kwenye ule udhaifu wako au kuufanyia kazi kwasababu huo ni udhaifu na mara Nyingi huwezi kubadili ila unaweza tu kudhibiti. Tumia muda mwingi Zaidi kwenye vile vitu ambavyo uko vizuri na utajikuta unaweza kushinda kile ambacho kinakufanya uanguke kirahisi.
Ubarikiwe sana,
Rafiki Yako, Jacob Mushi