HATUA YA 4; Fanya Kitu

jacobmushi
2 Min Read
Hakikisha siku haipiti hujafanya kitu katika kufikia ndoto na maono yako.
Kila unachokifanya kinasababisha matokeo baadae hivyo Hakikisha siku haipiti hujafanya chochote katika ile ndoto yako.
Ghorofa yenye floor 50 huanza kujengwa msingi na hujengwa kidogo kidogo kila siku hadi picha kamili ya jengo huonekana. Usikubali hata siku moja ipite kwako hujafanya chochote katika zile ndoto zako. Na unachokifanya kiwe kinafanya ukuaji wa ndoto.

Mfano hai: Hata kama unataka kujenga nyumba nzuri sana halafu tayari una kiwanja unaweza kuwekeza kidogo kidogo kwa kununua vile vitu vya muhimu zaidi. Unaweza kuanza kununua bati ukaziweka ndani, hata kama pesa ni kidogo ukisema ununue bati moja kila mwezi kwa mwaka unakuwa umenunua bati za kutosha. Hivyo unaweza kuanza kidogo kidogo kwa kila unachotaka kufanya.

Tatizo kubwa wengi wanapenda kujitetea kw sababu ambayo hawana namna ya kuitatua. Mtu anasema hana mtaji wa kuanza biashara fulani, ukimuuliza kwahiyo una mpango gani wa kupata mtaji hana.
Suluhisho: Tafuta namna yeyote ile ya kuanza. Wekeza kidogo kidogo hata kama hutaanza leo ili siku nyingine ukiulizwa kwanini huna cha kufanya sema nimejikusanya nina hiki.
Kama hujui kabisa jinsi ya kuanza kidogo kidogo tuwasiliane.
Karibu sana.
Jacob Mushi,
Entrepreneur & Author,
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com, www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading