HATUA YA 40: Unaondokaje Duniani?

jacobmushi
2 Min Read
“Tukijifunza kuacha historia njema kwa kutenda mema katika maisha ya wengine itatuwezesha tuondoke duniani tukitabasamu na huku tukiwaacha wengi wakitokwa na machozi”


Katika kitabu changu Kiitwacho Siri 7 za Kuwa Hai Leo  nimezungumzia juu ya kutengeneza historia mpya. Inawezekana umeshatenda mambo mengi mabaya kwenye maisha ya wengine kwa namna mbalimbali lakini kama bado upo hai una nafasi ya kufanya mambo mapya na kuacha alama mpya kwenye maisha yao.

Unaondokaje Duniani? Ukiondoka unaacha kitu gani nyuma yako? Watu wanasema nini juu ya ulichofanya kwenye maisha yao?
Tenga muda utafakari kuhusu hili kwani bado unayo nafasi ya kufanya mambo makubwa. Haijalishi unafanya kitu gani sasa hivi ukiamua unaweza kufanya sababu ya wewe kuacha historia ambayo itakuwa ni msaada wa vizazi vijavyo.

Yafanye maisha ya wengine yawe na furaha kupitia kile unachokifanya. Ni kweli huwezi kumridhisha kila mtu lakini kwa chochote unachokifanya lazima utapata wafuasi. Tumia nafasi hiyo kuwafanyia mambo bora kuliko mtu mwingine yeyote. Hapo ndipo kwenye mafanikio yako.

Jaribu kwenda hatua ya ziada kwenye kila unachokifanya. Usikubali kufanya mambo kwa namna ya kawaida tu. Kama unachokifanya kuna mtu mwingine anaweza kukifanya basi hakina maana sana. Tafuta utofauti wako ambao hakuna mtu mwingine anaweza kuuiga. Unacho kitu cha tofauti sana ndani yako.

Nguvu zipo ndani yako, uwezo upo ndani yako, tafuta maarifa kama haya uweze kutumia vyema vyote ulivyonavyo. Unaweza kuondoka duniani ukaancha alama kubwa na wengi wakajifunza nyuma yako.

Usiache kusoma Kitabu changu Siri 7 za Kuwa Hai Leo utagundua mambo mengi sana juu ya uhai wako.

Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading