Kwenye Maisha yetu siku zote kila mtu anatamani mabadiliko, kila mmoja anatamani kupata vitu Fulani kwenye Maisha yake. Ili ubadili chochote kwenye Maisha yako lazima ukubali kuchukua hatua.

Kama kweli Unakihitaji kitu utakitafuta. Na ukikitafuta kwa bidii utakipata. Mara nyingi unaweza kuonyesha hamasa kubwa sana ya kupenda mafanikio na unayazungumzia sana lakini hakuna unachofanya ili kukufikisha unakotaka.

Fanya maamuzi ya kuchukua hatua kwenye kile unachokitaka. Wengi wetu hatujaamua tuko nusu nusu kwenye vitu tunavyovifanya kwenye mahusiano tuliyonayo ndio maana siku zote hatufiki mahali.

Biashara inapokuwa ngumu kabla hujaamua kuiacha lazima ujiulize ni nani sababu ya kwanza kufanya biashara kuwa ngumu. Mara zote sababu ni wewe sasa kama wewe ndio tatizo la biashara yako unafikiri ukienda kuanza nyingine utapata mafanikio?

Kabla hujaamua kumuacha mpenzi wako, jiulize tatizo ni nini? Maana unaweza kusema ooh huyu ana tabia hii kumbe wewe ndie mbovu unafikiri utapata ambae yuko sawa wakati wewe ndie mbovu? Tatizo ni wewe anza kujirekebisha. Hakuna kitu kizuri kinachotokeaga vitu vizuri vinatengenezwa. Watu waaminifu hawakuzaliwa waaminifu wanatengenezwa. Watu wanaojua kupenda hawakuzaliwa wakijua kupenda wanatengenezwa. Kabla hujaenda kutafuta mwenye mapenzi ya kweli jiulize wewe unayo?


Kabla hujatafuta mwaminifu jiulize wewe ni mwaminifu? Halafu chukua hatua. Anza kubadilika wewe mwenyewe. Ukishabadilika ukaanza kuchukua hatua vitu vizuri vinakufuata. Vitu vinavyofanana na wewe vinaanza kuja.
Maisha ni ya kwako usipoamua kubadilika utabaki hivyo hivyo. Chochote unachokitaka kinakuja pale unapoamua kubadilika. Na mabadiliko huanzia ndani yako.
Soma kitabu change cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo.
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading