Yapo mambo mengi sana yanaweza kukuzuia au kukurudisha nyuma kwenye kutimiza ndoto yako lakini hayana uwezo wowote wa kuamua ushindwe. Jambo lolote unaloona linakuzuia wewe iwe ni changamoto au maneno ya watu siku zote hua hayana nguvu yoyote. Nguvu ya wewe kuacha hutoka ndani yako.


Usije kujitetea hata siku moja kwamba kuna watu walisababisha wewe ukashindwa kutimiza ndoto yako. Wewe mwenyewe ndio uliamua kutoka ndani. Watu wanaweza kukusema na kukucheka lakini hawawezi kukusaidia kuamua kutoka ndani.

Changamoto zinaweza kuwa ngumu sana lakini wewe ndie unaeamua kurudi nyuma. Usijitetee kwa namna yeyote ile nguvu ya kusonga mbele ipo ndani yako na nguvu ya kurudi nyuma ipo nyuma ndani yako.

Kitu kimoja tu ambacho hatuna uwezo wa kukizuia kwenye Maisha yetu ni Kifo. Kifo pekee ndio kina uwezo wa kukuzuia wewe usifikie kule unakotaka kwenda. Huna uwezo wa kuamua siku yako ya kufa. Huna uwezo wa kuamua ufe kifo cha namna gani labda ujiue.

Hiki ndio kitu kimoja ambacho kina nguvu ya kutukwamisha. Sasa kwasababu huna namna yeyote ya kuzuia kifo embu achana nacho. Wala usiwaze kwamba ukifa itakuaje sahau kwa muda komaa kwenye ndoto yako.
Moja ya jambo ambalo watu wengi wanapolifikiria huwa wanaogopa sana ni KIFO. Utashangaa kwanini leo nazungumzia Kifo ila hakuna namna nyingine lazima ufahamu maana kifo kipo siku zote. Usiwe na hofu kwenye jambo ambalo huna uwezo nalo kwa namna yeyote ile. Tumia muda mwingi kutumia nafasi ya uhai.

Kuna kanuni moja inasema kama kuna jambo linakuzuia wewe kutimiza ndoto yako litatue, kama huna utatuzi wake achana nalo. Hii kanuni itumie kwenye kifo maana kifo pekee ndio huwezi kukizuia.

Kama kuna jambo unalotakiwa ukomae nalo sana ni wewe kuacha alama kwenye dunia hii siku yeyote utakapoondoka duniani.


Namaliza kwa kusema HAKUNA KINACHOWEZA KUKUZUIA WEWE KUTIMIZA NDOTO YAKO ZAIDI YA KIFO. Mengine yote una uwezo wa kuyatatua. Mengine yote una nguvu ya kuyavuka.
Soma Kitabu change kiitwacho Siri 7 za Kuwa Hai Leo weka oda kwa kunitumia ujumbe kwenye namba 0654726668

Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading