Kabla Ya kumjua mteja ni muhimu pia ukatambua unauza nini? Maana kabla hujauza ni vizuri sana ujue bidhaa yako inakwenda kumgusa nani.
Kila binadamu hapa duniani kuna kitu anauza tatizo linakuja pale ambapo mtu hajui kama anauza. Na kama alisikia mahali kwamba anauza basi hajajua anauza nini.
Ili uweze kufikia mafanikio makubwa ni vyema utambue unauza nini. Kama wewe umeajiriwa basi unamuuzia mwajiri muda wako pamoja na ujuzi ulionao. Kama wewe una kipaji basi unauza kipaji chako. Chochote kile unachokitoa kwa ajili ya wengine na unapokea malipo basi unauza
Mteja wako ndio wa muhimu sana kuliko bidhaa yako. Kwani hata kama una bidhaa nzuri kiasi gani halafu haina wateja hakuna maana ya kuwa nayo.
Je unamjua mteja wako?
Mteja wako Yuko wapi?
Kama humjui mteja wako unaweza kukata tamaa haraka sana. Mfano umeanzisha biashara yako halafu ukaenda kuwauzia watu kama mia moja hivi kumbe katika wale watu mia wateja wako ni watatu tu. Umefika pale ukapiga kelele weee! Mwisho wa siku wakajitokeza watatu tu wakanunua. Utarudi nyumbani ukisema biashara ngumu kumbe hukwenda kwa wateja wako.
Unajua sababu inayomfanya aje kununua hapo kwako au hicho unachokitoa?
Ili uweze kuuza vizuri lazima uingie ndani Zaidi ujue bidhaa yako inakwenda kumsaidia kwa kiasi gani mteja wako. Kama haimsaidii hakuna haja ya wewe kuendelea kumuuzia.
Kama una wateja watano ukiwahudumia vizuri watakuwa mabalozi wazuri sana wa huduma yako au bidhaa yako na watakuletea wenzao uwatatulie shida zao.
Ili uweze kufikia ndoto yako hakikisha unawahudumia wateja wengi Zaidi. Unaanza kidogo kidogo hadi unafikia ndoto yako.
Usiache kusoma kitabu change cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo. Weka oda yako kwenye namba 0654726668
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com, www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.