HATUA YA 46: Ukweli Utakuweka Huru.

Kuna msemo mmoja unasema ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu.

Walisema hivi kwa sababu ukidanganya halafu ukasahau ulichodanganya huwezi kuwa huru.

Ukidanganya mara ya kwanza itakubidi udanganye mara ya pili.

Uongo ni tabia mbaya sana ndio maana ulipokuwa mdogo ulichapwa sana pale ulipodanganya.

Ukweli Utakuweka Huru kwa sababu huna haja ya kukumbuka ulichokisema. Mara zote unapokuwa mkweli huwezi kuwa na mambo ya kufichaficha.

Kuwa mkweli kwa watu wanaokuzunguka. Kuwa mkweli haimaanishi uwe wazi kwenye kila kitu chako. Kuwa mkweli kunafanya mtu asiwe na wasiwasi na wewe.

Matatizo mengi ya sasa yanaletwa na watu wengi kuwa waongo. Uongo kwenye jamii zetu, familia, serikali,  na sehemu mbalimbali za kazi.

Ndugu yangu kama unataka kuishi maisha yenye amani na furaha hapa duniani kuwa mkweli tu. Uongo utakutesa, Uongo utakufanya uishi maisha ya wasiwasi.

Jiondoe kwenye kifungo cha Uongo uwe huru. Kama kuna watu uliwadanganya nenda katafute uhuru wako kwa kusema kweli.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,

This entry was posted in HATUA ZA MAFANIKIO on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *