Katika Kitabu Cha Think and Grow Rich Mwandishi Napoleon Hill (FAITH and FEAR) Where the one is found the other cannot exist) Imani na Hofu, Popote utakapokutana na kimojawapo kingine hakiwezi kuwepo.
Kama wewe una hisia za hofu siku zote huwezi kuwa na Imani. Hofu ndio imevunja mahusiano mengi, hofu imewafanya watu waache kuwa na ndoto kubwa. Hofu imewafanya watu waogope kuoa na kuolewa.
Hofu inahusika kwa kiasi kikubwa sana pale mtu anapotakiwa kufanya maamuzi. Wakati mtu anapotakiwa kufanya maamuzi kuna Hofu inakuja ndani yake juu ya jambo ile analotaka kuamua.
Wengine wamekuwa na ndoto kubwa sana lakini hadi sasa hakuna walichokifanya. Wengine wameishia kuandika mawazo yao mazuri ya Biashara lakini wakaogopa kuchukua hatua yeyote.
Hofu ni hisia tu zilizopo ndani yako zinazokutisha juu ya vitu Fulani ambavyo kiuhalisia havipo. Unapotaka kuingia kwenye mahusiano mapya unapata hofu labda na huyu atanisumbua kama yule mwanzo. Ukweli halisi ni kwamba binadamu hawafanani na mambo hayatokei kama tunavyoyapaia hofu.
Unapotaka kuanza biashara unapata hofu ya kushindwa lakini ukweli kushindwa hakupo. Inawezekana pia unapata hofu na woga wa kusimama mbele za watu siku moja lakini ukweli hiyo ni hofu tu na haina ukweli wowote.
Zikatae hofu kwasababu ndio zinaongoza kuua Imani yako. Hofu zinaletwa na watu ambao wamekuzunguka. Marafiki zako wanaweza kuwa chanzo cha hofu. Ndugu zako wa karibu kabisa wanaweza kuwa chanzo cha hofu. Habari unazofuatilia mara kwa mara zinaweza kuwa chanzo cha hofu.
Kama wewe unakaa mara zote unasoma habari za watu waliochana kwenye mahusiano lazima ujae hofu ya kuingia kwenye mahusiano au ndoa. Kama wewe unatumia muda mwingi kufuatilia habari hasi juu ya chochote kile lazima ujae hofu.
Soma: Ukweli Utakuweka Huru
 Jitengenezee namna bora ya kuepuka hofu zinazoingia ndani yako. Kaa na washindi, jichanganye na watu walioshinda na wanaofanya vizuri. Hawa ndio wanaweza kukutia moyo wewe usonge mbele.
ISHINDE HOFU.
 Usiache kusoma Kitabu changu Siri 7 za Kuwa Hai Leo

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading