Muda ndio bidhaa ya thamani kuliko bidhaa ya yeyote hapa duniani. Mtu akikupa kila unachokihitaji kwenye dunia halafu akakunyima muda vyote alivyokupa vinakuwa havina maana.
Muda ndio Maisha yetu tunayoishi. Muda ndio Maisha yetu! Naweza kusema Miasha yetu yamefungwa ndani ya muda. Hakuna anaejua anakuwepo hapa duniani kwa muda gani. Wengine wameondoka wakiwa wadogo tukabaki tunashangaa na huzuni kubwa ndani yetu.
Wengine ni wazee sana hawawezi kuona wala kutembea sasa lakini bado ni wazima wanaishi. Jambo la unalotakiwa uweze kulipigania kuliko linguine lolote ni muda wako.
Kama kuna mtu anauchezea muda wako ni kwamba hayajali Maisha yako mtu huyo sijui atakuwa anachezea muda wako kwa namna gani lakini huyu mtu anacheza na Maisha yako.
Muda ambao utakuja kuujutia kuliko mwingine wowote ni ule uliokuwa na watu wasio ongeza thamani yeyote kwenye Maisha yako. Watu hawa badala ya kukufanya wewe usonge mbele wamekuwa wakikunyonya hata kile kidogo ulichonacho. Wamekufanya mtumwa hata kuachana nao huwezi unaona kama kuna kitu kikubwa utapoteza.
Nikwambie ukweli umeshapoteza na unaendelea kupoteza muda ambao ni Maisha yako. Kila sekunde unayoitumia hovyo hapa duniani inaondoka kwa machozi. Kila dakika unayotumia kufanya mambo ya kijinga na yasiyojenga au kubadilisha Maisha yako au ya wengine utakuja kuijutia siku moja.
Kitu cha kuogopa sana ni kwamba muda haurudi nyuma tena. Kama ulipata muda Fulani wa kuonyesha ulivyo bore kwenye nafasi Fulani uliyoishikilia muda ukipita ni umepita. Nafasi hiyo unaweza usiipate tena au ukiipata basi tayari utakuwa umeonekana wewe ni mzembe.
Utakuja kujuta kupoteza muda wako mwingi kwenye vitu ambavyo havina mchango wowote kwenye Maisha yako na hii inaweza kukuta ukiwa kaburini au ukiwa sehemu ambayo huwezi tena kurekebisha kule ulipopoteza.
Embu mtazame mtu aliepo kitandani amevunjika miguu yote kwa ajali ya pikipiki mtu huyu alishapigiwa kelele sana juu ya uendeshaji mbovu wa pikipiki. Lakini mtu huyu hakusikia. Akaona kama anaonewa. Akaona kama anaingiliwa kwenye mambo yake binafsi. Mwisho wa siku mtu huyu yupo kitandani hana tena miguu. Kile alichozani hatendewi haki kumbe alikuwa anatendewa haki kuambiwa aendeshe kistaarabu.
Majuto ni Mjukuu. Kwa maana kwamba Majuto ni matokeo yanayokuja baadae. Vitu unavyofanya sasa vinaweza kukuletea majuto au furaha sana kwenye Maisha yako ya mbeleni.
Karibu sana.
Soma Kitabu Changu Siri 7 za Kuwa Hai Leo 0654726668
Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255654726668
Email: jacob@jacobmushi.com